KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 28, 2014

Yanga yapata ahueni ya ushindi dhidi ya Prisons uwanja wa Taifa ilhali Kagera Sugar wakiibuka wababe mbele ya JKT Ruvu uwanja wa Chamazi.

Mfungaji wa goli la kwanza la Yanga Kiungo Andry Coutinho
Yanga ya Dar es Salaam hii leo imefanikiwa kupata ushindi wa bao 2-1katika mchezo wa roundi ya pili ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga iliandika bao la kwanza kunako dakika ya  34 kupitia kwa kiungo Andrey Coutinho aliyepiga mpira wa moja kwa moja wa adhabu.

Prisons iliandika bao la kusawazisha katika kipindi cha pili dakika ya 66 kupitia kwa Ibrahim Kahaka kabla ya Yanga kuandika bao la pili lilifungwa na Simon Msuva.  

Kwa ujumla Yanga haikuwa katika kiwango kizuri kimchezo licha ya Tanzania Prisons kucheza wakiwa pungufu kuanzia dakika za mapema za kipindi cha pili kufuatia mlinzi wao mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu ambayo ilitokana na kadi ya pili ya njano.
 
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuanza kuhesabu alama tatu za kwanza katika ligi kuu msimu baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza na Mtibwa katika mchezo ulipigwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro wiki iliyopita.

Yanga sasa inajipanga kwa mchezo mwingine Oktoba 5 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani mchezo ambao utachezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo mwingine uliofanyika uwanja wa Chamazi Complex hii leo umeshuhudia wakata miwa wa Kagera timu ya  Kagera Sugar ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.

No comments:

Post a Comment