KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 26, 2014

Luis Suarez alalamikiwa kuwa bonge kabla ya kumaliza adhabu yake

Luis Suarez aliitwa kila aina ya majina alipokuwa katika klabu ya zamani ya Liverpool, lakini hakuwahi kuitwa bonge.

Televisheni ya jijini Madrid imemtaja mshambuliaji kuwa ni mwenye uzito kupindukia na kulalamikiwa kuwa anaonekana ni kama mchezaji mstaafu katika taarifa iliyorushwa mchana wa alhamisi siku ambayo Suarez alifunga magoli mawili katika mchezo wa kirafiki akiichezea Barcelona B dhidi ya kikosi cha Indonesian U19.
 
Ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya mchezo wa watani wa jadi Clasico katika msimu huu mchezo ambao utakuwa unaashiria kumalizika kwa adhabu ya mshambuliaji huyo kufuatia kumng'ata mlinzi wa timu ya taifa ya Italia mambo yanaonekana kumuendelea kombo nchini Hispania.

Bosi wa Barcelona Luis Enrique amejibu lawama hizo katika mkutano wake na waandishi wa habari akionekana kushangazwa na tuhuma hizo kwa Suarez