KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 19, 2014

Brendan Rogers amtetea Mario Balotelli licha ya kuendelea kushindwa kufunga magoli

Brendan Rogers amtetea Mario Balotelli licha ya kuendelea kushindwa kufunga magoli
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers ametetea Mshambuliaji wake Mario Balotelli baada ya kushindwa kufunga goli kwa mara nyingine tena katika mchezo wa ligi ya England dhidi ya QPR hii akisema mshambuliaji huyo hakusajiliwa kuziba pengo la Luis Suarez.
Suarez raia wa Uruguay alijiunga na Barcelona kiangazi kwa pauni milioni £70 mpango ambao ulipelekea Rogers kulazimika kumsajili Balotelli kutoka katika klabu ya AC Milan kwa pauni milioni £16 katika kujaribu kuziba pengo la Suarez aliyekuwa mfungaji bora wa Premier League msimu uliopita.
Hata hivyo hii leo, Balotelli alipata nafasi nzuri ya kufunga goli akiwa umbali wa yadi sita wakati kikosi cha Liverpool kikiangamiza kikosi cha Harry Redknapp kwa bao 3-2, huku pia wakikosa nafasi kadhaa.
Bado Rodgers amesisitiza kuwa "ni mchezaji tofauti na Suarez, na kusisitiza kuwa Balotelli ambaye ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji ambaye yuko 'on fire' kwasasa katika kikosi cha Southampton, Graziano Pelle atafunga tu magoli akiwa ndani ya himaya ya Anfield.

No comments:

Post a Comment