KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 19, 2014

Diego Costa kurejea uwanjani katikati ya mwezi Novemba huku Mourinho akishindwa kuweka wazi

Diego Costa kurejea uwanjani katikati ya mwezi Novemba
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hana hakina ni lini mshambuliaji wake Diego Costa atakuwa saswa kurejea uwanjani katika kikosi chake licha ya kusema tu kuwa anaweza kuichezea Hispania ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
Costa mwenye wa miaka 26, amefunga magoli tisa katika michezo saba ya ligi tangu ajiunge nayo kwa uhamisho uliogharimu klabu yake kiasi cha pauni milioni 32 akitokea katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispania lakini akiukosa mchezo wa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Crystal Palce kutokana na kupata majeraha.
Mourinho amesema "atakuwa katika hali nzuri katika kipindi cha katikati ya mwezi Novemba akirejea katika timu ya taifa. Hilo lina uhakika.
"atachezea kikosi changu atakapo rejea kutoka katika majukumu ya kimataifa" 
Mourinho Hapo kabla alionyesha hisia zake kufuatia kuchaguliwa kwa Costa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania akidai kuwa alikuwa hafanyi kitu chochote katika mazoezi na kwamba alipaswa kupatiwa matibabu kuliko kumuongezea michezo ya kucheza.

 

Michezo aliyocheza Costa akiwa na Chelsea

Burnley 1-3 Chelsea - Alifunga 
Chelsea 2-0 Leicester - Alifunga
Everton 3-6 Chelsea - Alifunga magoli mawili
Chelsea 4-2 Swansea - Alifunga magoli matatu
Chelsea 1-1 Schalke -Hakufunga
Man City 1-1 Chelsea - Hakufunga 
Chelsea 2-1 Bolton - Hakufunga
Chelsea 3-0 Aston Villa - Alifunga
Sporting Lisbon 0-1 Chelsea - Hakufunga
Chelsea 2-0 Arsenal -Alifunga