KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 30, 2014

Javer Mascherano mchezaji bora wa mwaka Barcelona

Javer Mascherano ametajwa kuwa mchezaji bora wa Barcelona kwa msimu wa 2013-14.

Lionel Messi alishinda tuzo hiyo kwa miaka mitatu katika kipindi cha miaka minne iliyopita mbayo inakwenda kwa jina la 'Memorial Aldo Rovira' ambapo sasa amezidiwa na muajentina mwenzake  ambaye ameimarisha ubora wa safu ya ulinzi ya 'Blaugrana' katika msimu uliopita licha ya kushindwa kutwaa taji lolote msimu huo.

"nawashukuru wote ambao wamenipigia kura na kupelekea kupewa tuzo hii," amenukuliwa Mascherano na mtandao wa klabu yake

"tutaendelea kufanya mambo kwa kujitoa tukijaribu kuendelea kuwa watiifu kama ambavyo klabu yetu inatutaka."

Tuzo hiyo imepewa jina hilo kufuatia Aldo Rovira, ambaye alikuwa ni mwanachama maarufu wa klabu hiyo ambaye alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2009. Ili kumpata mshindi wa tuzo hiyo, watu mashuhuri kutoka Barcelona na vyombo vya habari kutoka Katalunya wanapiga kura.

Mascherano mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani alijiunga Camp Nou akitokea katika klabu ya Liverpool mwak
a 2010.