KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 22, 2014

Liverpool sasa wamgeukia Ezequiel Lavezzi kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya Mario Baloteli kushindwa kuziba pengo la Suarez

Liverpool imesema wanajitayarisha na mpango mpya wa pauni milioni £30 kwa ajili ya kuopata huduma ya nyota wa Paris Saint-Germain, Ezequiel Lavezzi katika usajili wa mwezi Januari.
Wekundu hao wamekuwa wakihusishwa na mshambuliaji huyo katika sehemu kubwa ya kipindi cha uhamisho wa wachezaji cha kiangazi lakini mpango huo ulikwama.
Hata hivyo kwa mujibu wa Fichaje, bosi wa Liverpool Brendan Rodgers anajipanga kuujaribu tena mpango huo kwa mabingwa wa soka wa nchini Ufaransa wakati dirisha la usajili litakapo funguliwa tena mapema mwakani.
Liverpool imekuwa ikihaha kusaka mshambuliaji tangu mapema ilipoanza kampeni za msimu mpya ambapo kwasasa Daniel Sturridge bado ni majeruhi na Mario Balotelli aliyesajili kiangazi bado hajaonyesha makeke yake ndani ya Premier League tangu ajiunge na klabu hiyo.
LIverpool iko katika nafasi ya sita katika ligi ikiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea kwa alama tisa baada ya michezo minane kukamilika.
Lakini Rodgers bado ana matumaini ya kuimarihsa kikosi chake mwezi Januari ili kuweza kupata nafasi nyingine ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu mwingine.