KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 1, 2014

Ethiopia yajitoa kuandaa michuano ya Chalenji 2014 na huenda yakaelekea Sudan

Mwenyekiti wa cecafa Leordigar Tenga kushoto na katibu mkuu wake Nicolaus Musonye

Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) kwasasa linaangalia uwezekano wa kupata muandaaji mpya wa michuano ya mwaka huu 2014 ya chalenji kufuatia Ethiopia kujitoa.
Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye ameuthibitishia mtandao wa Rockersports kwa njia ya simu kutoka Nairobi, Kenya kuwa Ethiopia imejitoa.

“Ethiopia imetuandikia na kusema hawako katika nafasi ya kuandaa michuano hiyo,” Musonye amesema na kuongeza kuwa CECAFA imekubali kujitoa kwao
“hatuna la kufanya zaidi ya kukubali ombi la lakini tayari tumeanza kazi ya kusaka mwenyeji mpya.”
Musonye amethibtisha hilo licha ya shirikisho la soka la Ethiopia EFF kuwaandikia wakiwa wamechelewa, lakini amesema kuwa michuano hiyo itafanyika kwa tarehe iliyotajwa kati ya Novemba na Desemba na kwamba mwenyeji mpya atatangazwa wiki iyayo.
"Sudan yuko tayari akingojea hivyo michuano inaweza kuelekea Khartoum, lakini tutatangaza baadaye wiki ijayo"
Mwaka uliopita 2013 michuano hiyo ilifanyika nchini Kenya ambapo wenyeji walitwaa taji hilo baada ya kuifunga Sudan katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Nyayo jijini Nairobi.

No comments:

Post a Comment