KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 5, 2010

Danny Jordaan anatafuta kazi ya utendaji Fifa Danny Jordaan ambaye alikuwa ni mtendaji mkuu wa fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini anajipanga kuelekea kuomba kazi ya utendaji ndani shirikisho la kandanda duniani fifa.
Jordan mwenye umri wa miaka 59 mzaliwa wa Afrika kusini ameteuliwa na nchi yake kwa nafasi hiyo ya utendaji nafasi ambayo uchaguzi wake utafanyika mwakani.
Akikaririwa Jordaan ambaye sasa anajipanga kuzunguka katika bara zima kuomba kampeni za kuungwa mkono miezi michache ijayo anasema
"kusimamia kombe la dunia ni msaada mkubwa ,"
Ameongeza kwa kusema
"ni muhimu kwangu kwamba Africa inadhani kuwa nitatoa msaada."
Nafasi mbili kati ya nne za utendaji ndani ya Fifa zitakuja katika uchaguzi wa awali wa fifa ambao umepangwa kufanyika mwezi February.
Nafasi moja kwasasa inashikiliwa na Mnigeria Amos Adamu,ambaye amesimamishwa kufuatia shutuma za kutanga hongo ili kuuza kura yake ya maamuzi ya nani wa kuandaa fainali za kombe la dunia kwa miaka ya 2018 na 2022.
Nafasi nyingine ya Afrika ndani ya fifa kwasasa ainashikiliwa na Jacques Anouma, Rais wa shirikisho la kandanda la Ivory coast , ambaye bado hajatangaza hadharani kama atatetea nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne.
Adamu anatarajiwa kuendelea kushikilia nafasi yake kama atasafishwa na na kamati ya maadili ya juu ya tuhuma zake za hongo mwezi ujao.
Mwisho wa kutoa mapendekezo ya majina ya wale wanao wania nafasi hizo ni November 23, ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kikao cha uchaguzi cha shirikisho la kandanda barani Afrika CAF kitakacho fanyika katika jiji la Khartoum nchini Sudan.
Jordaan ndiye wa kwanza kuonyesha dhamira hiyo.
Uzoefu wa Jordan kuongoza mpira umedhihirisha wazi kwa miaka 20 iliyopita yaani miongo miwili iliyopita ikiwa ni pamoja kushiriki kwa mafanikio katika maandalizi ya kombe la dunia jambo ambalo linaweza kumpa mafanikio

No comments:

Post a Comment