KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 9, 2010

FA yakataa rufaa ya kadi nyekundu ya Mario Balotelli
Mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli imethibitishwa kuwa atakosekana kwa michezo mitatu baada ya chama cha kandanda cha nchini Uingereza FA kuikataa rufaa ya timu yake kutaka adhabu dhidi yake itenguliwa kwani mshambuliaji wao hakustahili adhabu hiyo baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya West Brom.

nyota huyo wa kimataifa wa Italia alionyeshwa straight red card baada ya kumparamia kwa makusudi Youssuf Mulumbu katika mchezo ambao City ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0.

Balotelli mwenye umri wa miaka 20 atakosekana katika mchezo muhimu maarufu kama Manchester derby jumatano hii dhidi ya Manchestwer united kule eastland lakini pia atakosekna katika mchezo dhidi ya Birmingham City jumamosi na mcjhezo mwingine dhidi ya Fulham jumapili ijayo.

katika mchezo aliopewa kadi nyekundu alifunga mabao yote mawili ya ushindi kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Taarifa ya FA imesomeka "At a Regulatory Commission hearing today, a claim that the standard punishment is clearly excessive from Manchester City's Mario Balotelli was dismissed.

No comments:

Post a Comment