KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 19, 2010

Rooney kuwepo kikosini United dhidi ya Wigan Sir Alex Ferguson ametanabaisha kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney "huenda akawepo katika benchi hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya kandanda nchini Uingereza dhidi ya Wigan.
Rooney amekuwa nje ya dimba kwa mwezi mzima baada ya tatizo la ankle akiwa mazoezini mwezi October,ambapo baada ya matatizo hayo alianza kuweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka Old Trafford kabla ya kuipindua dhamira yake hiyo na kuingia mkataba wa miaka mitano .
United imechomoza na ushindi katika michezo sita na kwenda sare michezo miwili michezo ambayo yote Rooney hakuwepo kikosini lakini baada ya matokeo hayo katika michezo dhidi ya Manchester City na Aston Villa, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza tanatakiwa aonyeshe uwezo na kuwa msaada ndani ya kikosi .

Amerejeea Old Trafford juma lililopita baada ya kuwepo nchini Mrekani katika mazoezi ya kurejesha ufiti wake katika makao makuu ya NIKE huko Portland, Oregon licha kurejea kwake nchini Uingereza lakini bado kurejea katika mazoezi huku meneja wake Ferguson akisema Rooney huenda akawepo dimbani hapo kesho dhidi ya Wigan.

Jermain Defoe ametajwa katika kikosi cha Tottenham Squad kuelekea katika North London Derby dhidi ya Arsenal
Jermain Defoe amejumuishwa katika kikosi cha timu yake ya Tottenham Hotspur kuelekea katika north London derby dhidi ya Arsenal.
Mshambuliaji huyo amekuwa katika maumivu ya ankle akiwa katika mchezo wa kimataifa wa kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya 2012 dhidi ya Switzerland mapema msimu huu .
Katika hatua nyingine mshambuliaji huyo wa zamani wa Portsmouth ameonekana kupata nafuu na kurejea katika mazoezi mapema juma hili .
Defoe amerejea katika kipindi muafaka kwani baada ya mchezo mchezo wa dhidi ya Arsenal kule Emirates watafuatiwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya mabingwa wa udachi FC Twente,na kasha wakirejea nyumbani watakuwa na kazi nyingine dhidi ya Liverpool.


Meneja wa uingereza Fabio Capello ansema atazungumz na meneja wa Liverpool Roy Hodgson juu ya maumivu ya Steven Gerrard
Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesisitiza kuwa atafafanya mazungumzo na meneja wa Liverpool Roy Hodgson juu ya Steven Gerrard juu ya kumtumia kwa muda mrefu katika mchezo ambao Uingereza ilipoteza kwa ufaransa nyumbani jumatano.
Liverpool ilitoa angalizo kwa meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Capello kutokumtumia nahodha wao Gerrard kwa zaidi ya dakika 60 laikini bosi huyo wa zamani wa Real Madrid aliamua kumchezesha mpaka akakamatwa na msuli
Maumivu ya nahodha huyo wa Liverpool sasa yatamgharimu kuwepo nje ya dimba kwa kipindi cha wiki nne lakini pamoja na yote bosi wa simba watatu yaani Uingereza Capello bado hajaomba radhi mpaka sasa kukiuka makubaliano .

MANCHESTER UNITED NEWS
Schmeichel ana wasiwasi juu ya kiwango cha Lindegaard


Mlinda mlango wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel anaamini mlinda mlango Anders Lindegaard hana ubora kiasi kuaminiwa ndani ya klabu yake .
Maafisa toka katika klabu yake mlinda mlango huyo Lindegaard klabu ya Aalesunds, kwasasa wako huko Manchester katika mipango uhamisho wa mlinda mlango huyo mpango wa gharama ya pauni milioni 3.5 na inaarifiwa kuna harufu ya mafanikio
Lindegaard kwasasa ana umri wa miaka 26 na ndiye mlinda mlango nambari moja wa Denmark lakini haja wahi kuwa katika kikosi cha kwanza mpaka alipo elekea huko Norway mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment