KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 5, 2010

Samson Siasia ameteuliwa kuingoza Nigeria super eagles Nigeria imemtangaza Samson Siasia kama kocha wao mpya wa timu ya taifa huku taratibu za kumpatia mkataba wake wa miaka minne ijayo zikitarajiwa kukamilishwa masaa 48 yajayo
Siasia mwenye umri wa maiaka 43 ambaye alikuwa ni mshambuliaji wa Super Eagles striker ameteuliwa kuingoza timu ya taifa lake baada ya kumshinda nahodha wa zamani wa timu hiyo Stephen Keshi kufuatia maamuzi ya kamati ya ufundi ya soka la Nigeria kukutana hapo jana
Siasia ambaye amekuwa akiitumikia timu ya taifa ya Nigeria yenye wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 iliyoshiriki Olympic atakuwa anachukua nafasi ya mtangulizi wake ambaye alikuwa akiikochi timu hiyo kwa muda kocha raia wa Mali Austin Eguavoen.
Siasia anatarajiwa kuanza kazi rasmi December mosi na kwasasa moja ya majukumu yake makubwa ni kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika za 2012.

Taarifa za kupitishwa kwa siasia zimetolewa hapo jana na shirikisho la kandanda la Nigeria (NFF)

No comments:

Post a Comment