Jordi Alba |
Barcelona imetangaza
kupitia mtandao wa klabu hiyo imekubali kulipa ada ya kumsajili mchezaji wa Valencia
Jordi Alba.
Kwa muda
muda mrefu Barca maarufu kama Blaugrana imekuwa ikihusishwa kutaka huduma ya
mlinzi huyo wa kushoto na sasa imebakia hatua ya mwisho ya kukamilisha usajili
huo baada ya mazungumzo ya kina na kukubaliana kulipa ada ya uhamisho ya euro
milioni €14.
Alba anatarajiwa
kufanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo na kusaini mktaba wa miaka mitano endapo
atafanikiwa kipimo hicho.
Taarifa kupitia
mtandao wa klabu hiyo imesema
"Barcelona
inatangaza kuwa leo tumefikia makubaliano na Valencia juu ya uhamisho wa Jordi
Alba kilichobaki ni kipimo cha afya ambacho kitafanyika wiki ijayo" .
"gharama
ya uhamisho wake ni euro milioni €14 na mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka
mitano."
Alba ambaye
kwasasa ana umri wa miaka 23, ni zao la Barcelona kupitia kituo chao cha kukuza
vipaji “youth academy” lakini alishindwa kuingia katika kikosi cha kwanza Camp
Nou na kuondoka mwaka 2005.
Sasa atakuwa
akirejea nyumbani alikokulia baada ya kucheza klabu kadhaa kama Cornella,
Gimnastic na Valencia.
No comments:
Post a Comment