Sports Club
Villa ya nchini Uganda imeanza kufikiria kufaidika na malipo ya uhamisho wa
mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ambaye kunataarifa kuwa huenda akauzwa na
Simba katika klabu moja ya nchini Italia kama si Orlando Pirates ya Afrika
kusini.
Hata hivyo mchezaji huyo anatarajia kuelekea nchini Italia kwa majiribio ya wiki mbili hizi zikiwa ni taarifa toka kwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange Kaburu
Klabu hiyo
kwasasa inafikiria kupata si chini ya shilingi milioni 100 za Uganda endapo mauzo
ya mchezaji huyo yatafikia shilingi bilioni 1.6 kwa fedha za Uganda fedha
ambazo Simba inatazamia kulipwa endapo atajiunga na Orlando Pirates.
Endapo mchezaji
huyo wa kimataifa wa Uganda ambaye kwasasa ndiye mfungaji anayeongoza katika
timu ya taifa ya Uganda Cranes akiwa na magoli mawili katika michezo mitatu
aliyoichezea timu ya taifa atauzwa Villa nayo itakuwa ikikinga mkono kusubiri
malipo ya mauzo yake.
Kwa mujibu wa taarifa toka nchini Uganda
ambazo zimenukuliwa katika mtandao mmoja wa michezo wa Ugandasport.org zimesema
faida kama hiyo ni kawaida kwa klabu ambayo mchezaji amepitia kabla ya kuuzwa
na klabu yake anayoichezea na kusema ni utaratibu mpya uliowekwa na kuheshimiwa
na FIFA.
Taarifa za
nyuma zilinukuu wakuu wa Simba wakisema wanatarajia kumuuza Okwi kwenda Pirates
ya Afrika kusini kwa zaidi ya shilingi milioni 800m ukilinganisha na shilingi
milioni 12 ambazo Simba iliilipa Villa wakati wakimnunua.
Mwaka jana Okwi
alijaribu kucheza soka katika klabu ya Kaizer Chiefs kabla ya msimu uliopita
lakini aligoma kuelekea huko na badala
yake akaelekea kujaribu soka nchini Uturuki ambako alishindwa kufuzu.
No comments:
Post a Comment