Timu ya
utabibu ya Real Madrid imemnyooshea Cristiano Ronaldo alama ya kijani kwenda
Ureno kuripoti kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.
Mshambuliaji
huyo hatari alikuwa katika maumivu ya bega katika mchezo huo wa jana wa ligi
kuu ya soka nchini Hispania La Liga ambapo Madrid ilikwenda sare ya mabao 2-2 na
Barcelona mchezo uliopigwa katika dimba la Nou Camp.
Kama hiyo
haitoshi , Ronaldo tangu jana usiku amekuwa akifanyiwa uangalizi na madaktari
wa Madrid akiwa nyumbani, na tayari mabingwa hao wa ligi ya Hispania wametangaza
kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa Ronaldo hajapatwa na maumivu makubwa.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 alitazamiwa kuelekea nyumbani Ureno mchana wa leo
kwa ajili ya jukumu la kimataifa ambapo Ureno inatarajia kucheza dhidi ya
Russia ijumaa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali ya kombe la dunia 2014
kabla ya mchezo mwingine dhidi ya Ireland ya Kaskazini siku nne baadaye.
Kiungo wa Manchester
City Barry: Siko tayari kustaafu soka la kimataifa
Kiungo wa Manchester
City Gareth Barry amesisitiza kuwa hayuko tayari kustaafu soka la kimataifa huku
akiwa na matumaini makubwa kuwa
atachaguliwa katika kikosi kitakacho tangazwa hivi karibuni, licha ya
kutokuwepo katika kikosi kilichopita ambacho kilicheza dhidi ya San Marino and
Poland.
Barry, ambaye
alifanya kazi kubwa katika timu yake ya City ambayo ilichomoza na ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Sunderland jumamosi, hajachaguliwa tangu mchezo wa kwanza wa
kirafiki wa kocha Roy Hodgson dhidi ya Norway mwezi May.
No comments:
Post a Comment