Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba ya jijini Dar es Salaam imeondoka jijini hii leo na kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya saba dhidi ya Coast Union ya huko mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Mkwakwani Oktoba 13.
Simba wameelekea Tanga wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo ya Tanzania Bara inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Simba wakiongoza baada ya kujikusanyia jumla ya alama 16 wakifuatiwa na Azam fc yenye alama 14.
Simba imeondoka bila ya wachezaji wake kadhaa muhimu akiwepo Mrisho Ngasa anayesumbuliwa na malaria kama ilivyo kwa Ramadhani Chombo Redondo ambaye naye anasumbuliwa na malaria.
Wengine walioachwa ni Haruna
Shamte ambaye anasumbuliwa na enka, Kiggi
Makassi mwenye matatizo ya goti pamoja na Abdalah Seseme na Waziri Hamadi.
Kwa upande wa mganda Emmanuel Okwi yeye anaelekea kwao Uganda kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.
Waliondoka ni wachezaji 22 ambao ni,
MAKIPA:Juma
Kaseja na Wilbert Mweta.
Walinzi: Chollo,
Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman
Keita.
Viungo: Kazimoto,
Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban.
Washambuliaji:Sunzu,
Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.
RATIBA RAUNDI YA 7
10.10.2012. | 43 LEO | KAGERA SUGAR | JKT RUVU | KAITABA | KAGERA | |
11.10.2012. | 44 | TOTO AFRICANS | YOUNG AFRICANS | CCM KIRUMBA | MWANZA | |
13.10.2012. | 45 | POLISI MOROGORO | AZAM | JAMUHURI | MOROGORO | |
13.10.2012. | 46 | TANZANIA PRISONS | JKT OLJORO | SOKOINE | MBEYA | |
13.10.2012. | 47 | COASTAL UNION | SIMBA | MKWAKWANI | TANGA | |
13.10.2012. | 48 | RUVU SHOOTINGS | AFRICAN LYON | MABATINI | PWANI | |
13.10.2012. | 49 | MTIBWA SUGAR | MGAMBO JKT | MANUNGU | MOROGORO | |
No comments:
Post a Comment