Thomas
Vermaelen anaamini kuwa Jack Wilshere ana uwezo wa kuwa mmoja kati ya viungo
hodari dunaini.
Kiungo huyo
alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 14 akisumbuliwa na maumivu ya enka na
mguu lakini amerejea akiwa vizuri katika kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji
wenye umri chini ya miaka 21.
Amenukuliwa na
mtandao wa klabu hiyo akisema Vermaelen akisema,
"unajua
alichokifanya katika msimu wake mzima wa kwanza akiwa na Arsenal, alifanya vitu
vikubwa sana”.
"kwa
upande wangu anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora kabisa duniani. Ana uwezo
mkubwa wa kufikia hapo.
"ninafuraha
sana amerejea sasa. Anafanya kazi ya kurejesha uwezo wake kama zamani na hilo
ni jambo muhimu. Nadhani baadaye ataibeba timu hii."
No comments:
Post a Comment