KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 29, 2012

PETER TINO AKABIDHI BENDERA KWA SERENGETI BOYS KABLA YA KUIVAA CONGO BRAZZAVILLE KULE CONGO.

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa "Taifa stars"  Peter Tino ambaye alikuwa mgeni rasmi  katika hafla ya kuwaaga Serengeti Boys akimkabidhi nahodha wa timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 Miraji Adam Seleman bendera ya taifa jana usiku tayari kwa safari ya kwenda Congo Brazzaville kwenye hoteli ya Itumbi iliyoko Magomeni, jijini Dar es salaam
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa "Taifa stars"  Peter Tino akiwausia wachezaji timu ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17  jana usiku kabla ya safari ya kwenda Congo Brazzaville kwenye hoteli ya Itumbi iliyoko Magomeni, jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Serengeti Boyz wakifuatillia hotuba za kuwaanga kabla ya kukabidhiwa bendera tayari kwa safari ya kuelekea Congo Brazzaville
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa Taifa Stars Peter Tino jana usiku aliikabidhi timu ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 Serengeti boys bendera na wosia kabla ya kuanza safari ya kuelekea Congo Brazzaville tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya vijana wenzao wa huko.

Tino ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo aliwaasa wachezaji hao kucheza kwa kujituma wakijua kuwa nyuma yao kuna watanzania wanawafatilia na ndio maana wamepewa bendera ya taifa kwa sababu wanaiwakilisha nchi.

"Nyie ni jeshi la Tanzania mnakwenda kupigana mkiwa tayari mmeshashinda nyumbani hivyo vyovyote mnatakavyofanyiwa nyie fikirie mchezo tu", alisema Tino.

Pia aliwaambia kwenye mchezo kuna mbinu chafu ambazo zinaweza kutumika ili kuwadhoofisha kisaikolojia ila wasilitilie maanani bali wafikirie mchezo.

"Mchezo wenu ni sawa na mchezo wetu tuliocheza 1980 dhidi ya Zambia na dakika ya 89 mimi niliwanyamazisha Wazambia mbele ya Rais Mugabe baada ya kufunga bao na kufanikiwa kufuzu mataifa ya Afrika, alisema Tino.

Akizungumza na wachezaji Rais wa Shirikisho la Soka nchini Leodgar Chilla Tenga aliwaasa wachezaji wakazingatie kile tu walichofundishwa na kocha kwani anajua mchezo huu utakuwa mgumu

Timu iliondoka na ndege ya shirika la ndege la Kenya na msafara wa watu 27, wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kocha wa timu hiyo, Jacob Michelsen alisema kuwa anajua nakwenda kucheza natimu bora ila wao ni bora pia kwani wana faida ya bao la nyumbani.

"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob

Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatokana kutokana na mashindano ya Copa Coca cola wanahitaji anagalau sare ili kuweza kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana na kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment