Koman Billi Keita. |
Mlinzi wa
kati wa klabu ya Simba mwenye mapafu mithili ya mbwa Koman Billi Keita amesema
ana imani kocha mpya wa klabu hiyo Patrick Liewig ambaye anatarajiwa kuingia
mkataba na klabu hiyi mara baada ya sikukuu ya Chrismass, atampa nafasi ya
kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba kwa kuwa ni falsafa ya makocha wa
Ufaransa ni mpira wa nguvu na kasi ya kurosha uwanjani.
Keita ambaye
hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kocha
aliyefungashiwa virago Milovan Circovich wakati wa uongozi wake wa benchi la
ufundi amesema kwake yeye ni faraja kuona Simba inamleta kocha mfaransa ambaye
ana imani wataelewana vizuri kwakuwa wanaongea lugha moja ya kifaransa.
Amesema
hakuwa kwenye nafasi ya kucheza wakati wa Milovan kwa kuwa alikuwa mgeni mno katika
kikosi cha Simba na pia hakuwa anaujua vizuri mpira wa Tanzania jambo ambalo
amesema kwa sio tatizo tena.
Keita
amesema anajiamini kuwa yeye ni mchezaji mkubwa sana kwani amecheza soka na wachezaji
wakubwa katika timu ya taifa ya Mali kama Mamadou Diara, Seidou Keita, Drissa
Diakite, Cedric Kante na Bakaye Traore jambo ambalo anasema limemkuza sana
kiwango chake na kujenga kujiamini.
Keita
amesema anaheshimu sana uwezo wa mlinzi Shomari Kapombe ambaye anaamini mlinzi
huyo kiraka mwenye uwezo wa kucheza eneo lolote katika sehemu ya ulinzi kwamba
ana uwezo mkubwa sana na anaweza kucheza soka popote duniani kwani.
“Kapombe ni
mchezaji mzuri sana, ana fanana na wachezaji wa Afrika magharibi wenye uwezo na
kasi naheshimu sana uwezo wake, anaisaidia sana sehemu ya ulinzi ya Simba”
Somari Kapombe. |
Mbali ya Kapombe, Keita anawasifia pia wachezaji wengine kama Mwinyi Kazimoto, Jonas
Mkude na Amri Kiemba ambao amesema wanacheza kwa kujituma na si wavivu wa
mazoezi.
Kabla ya
kujiunga na Simba, Koman Billi Keita amewahi kuvichezea vilabu vya Stade Malienne ya
Mali, Shooting Stars ya Nigeria, Jeanne D’arc ya Mali na Iran-Cave ya Iran.
Keita anasema ligi kuu ya soka Tanzania bara ligi ambayo ina wachezaji wengi wenye vipaji lakini soka linachezwa kwa uvivu kwa kuwa wachezaji wengi hawana malengo ya kucheza soka nje ya Tanzania.
"Unajua mchezaji wa Tanzania akienda Mali, Nigeria, Camerron, Nigeria, Ivory Coast, Benin na Ghana hawezi kupata timu ya daraja la kwanza kuchezea kwa kuwa kule ligi ni ngumu. mimi mwenyewe niliposema nakuja Tanzania walinicheka wenzangu kwakuwa Tanzania haijulikani"
"halafu kule watu wanafanya sana mazoezi na ndio maana wanaonekana wana nguvu na miili mikubwa iliyojengeka, sasa hapa ligi ikisimama kidogo wachezaji nao wanasimama, hii inanishangaza sana".
"Wachezaji wa kule wanataka kucheza Ulaya na ndio maana wanasafiri sana kwenda ulaya kujaribu bahati zao, lakini hapa hawafanyi mazoezi na hawataki kwenda nje, ni vigumu kupata maendeleo"
Keita amemtaka Haruna Moshi ambaye ni swahiba wake mkubwa akacheze soka ulaya, kwakuwa anakipaji sana na anacheza soka kwa kutumia akili.
Amesema haruna anacheza soka la akili licha ya kwamba hatumii nguvu na kwamba kuna nchi ambazo Haruna anaweza kung'ara sana kama vile Ufaransa na Hispania.
No comments:
Post a Comment