KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 20, 2013

ROGASIAN KAIJAGE AANZA KAZI KUIFUNDISHA TWIGA STARS AIMARISHA NIDHAMU

WACHEZAJI wa timu Taifa ya wanawake “Twiga Stars” wamemgaya kocha Rogasian Kaijage, waanza kutii masharti yake.

Wachezaji hao ambao walikuwa wanakata nywele kwa staili za ajabu na uvaaji wa surulia na pensi kwa staili ya mlegezo wameonekana kubadilika baada ya kuwa na kocha mpya kwenye kikosi chao.

Kaijage ambaye amerithi mikoba ya Boniface Mkwasa baada ya kubwaga manyanga mwaka jana alipoita timu hiyo alikaa nao kikao na kuwaeleza kuwa hatapenda kuona wachezaji hao wakivaa staili ambazo zinaleta picha mbaya kwa jamii.

“Niliwaambia mpira unahitaji uwe na adabu ili ufanikiwe hivyo niwaambia wabadilike kuanzia muonekana hadi uwanjani na ndio maana unawaoneka wamesuka vizuri na kubana nywele vizuri na kuvaa nguo sawasawa”, alisema Kaijage

Wachezaji wa timu timu hiyo wameonekana wakiwa nadhifu kuanzia kwenye mavazi hadi kichwani na wakifanya mazoezi kwa ari na kocha huyo anapokuwa anawaita wachezaji hao wamekuwa wakionekana wakikimbia kuwahi kufika na si kutembea na utani umepungua.

Meneja wa timu hiyo Furaha Francis amefurahishwa na kitendo cha kocha kuwaeleza ukweli wachezaji kuwa nidhamu inaanzia kwenye muonekano kwa jamii.

No comments:

Post a Comment