Mshambuliaji wa Paris Saint Germain Edinson Cavani amewashukuru mashabiki wa klabu yake ya zamani ya Napoli kwa kumpa sapoti huku akitumia ukurasa mzima katika gazeti moja la nchini Italia.
Cavani alijiunga na PSG kwa thamani ya pauni milioni £55 mapema kiangazi licha ya kuhusishwa na kutaka kuelekea katika vilabu vingi nchini England ambapo jana alianza kwa mara ya kwanza kuitumikia klabu yake mpya katika mchezo wa ligi kuu ya nchini Ufaransa mchezo ambao PSG ambao ni mabingwa watetezi wa taji walipokwenda sara ya bao 1-1 na Montpellier.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alitumia ukurasa mzima wa gazeti moja la nchini Italia Corriere dello Sport kwa kuweka picha ukurasa mzima ambayo iliambatana na ujumbe maamlumu kutoka kwake kwenda kwa mashabiki wa Napoli.
Ujumbe ulikwenda sambamba na picha hiyo ya Cavani ni huu
‘1,000
unforgettable days, 104 special moments lived with you. The Azzurri are
in my heart forever. Thank you for all the love. Thanks Napoli.’
No comments:
Post a Comment