KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 10, 2013

PARIS ST-GERMAIN YASHIKWA VILIVYO NA MONTPELLIER KIVUMBI CHA KWANZA LIGI YA UFARANSA.

Paris St-Germain imeanza kutetea taji lake waliloshinda msimu uliopita katika ligi kuu ya soka nchini Ufaransa kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Montpellier ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya Laurent Blanc ndani ya klabu hiyo.

Bosi huyo wa zamani wa Ufarasna Blanc ambaye amechukua mikoba ya Carlo Ancelotti majira ya kiangazi anazamiwa kutetea taji hilo msimu huu lakini kikosi chake kililazimika kufanya kazi ya ziada katika mchezo huo uliopigwa Stade de la Mosson.
 
Mlinzi wa kushoto Maxwell alisawazisha bao dakika 15 baada ya mapumziko kufuatia Remy Cabella kuwafungia Montpellier bao la uongozi dakika ya 11 ya mchezo.

Mshambuliaji aliyesajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo akitokea katika klabu ya Napoli, Edinson Cavani, alianzia benchi lakini alikaribia kuandika bao katika mpira wake wa kwanza kuunsa tangu aingie uwanjani kunako dakika ya 72 lakini mshambuliaji huyo mwenye thamani ya uhamisho ya pauni milioni £55 alishindwa kufanya hivyo baada ya kuzuiliwa vema na mlinzi Siaka Tiene.

Montpellier walisalia 10 uwanjani kufuatia mlinzi Abdelhamid El Kaoutari kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano zikiwa zimesalia dakika 18 mchezo kukamilika.

Hii leo Monaco, iliyotumia karibu pauni milioni £130 katika usajili wake majira ya kiangazi itakuwa ikiwafuata Bordeaux.

No comments:

Post a Comment