Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria Emmanuel Emenike na mlinzi Kenneth Omeruo wameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa Super Eagles kinachotarajiwa kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Afrika mchezo ambao umepangwa kuchezwa Agosti 14.
Emenike ametaka kusalia nchini Uturuki baada ya kuongeza mkataba wake wa kuendelea kuichezea klabu yake ya Fenerbahce.
Afisa habari wa shirikisho la soka la Nigeria NFF Ben Alaiya amenukuliwa akisema
"Ni mchezaji anayethaminika nchini Uturuki na ameomba aruhusiwe kusalia huko kwa ajili ya kujiweka vizuri na klabu yake"
Omeruo ambaye alipata majeraha ya bega katika michuano ya shirikisho ameambiwa aendelee kusalia na klabu yake ya Chelsea huku akiponya majeraha hayo.
Gege Soriola na James Okwuosa ambao wote wanacheza soka nchini Afrika kusini wameitwa kuziba mapengo ya wachezaji hao.
Emenike, ambaye alikuwa ndiye mfungaji mwenye magoli mengi katika kampeni za michuano ya mataifa ya Afrika amekuwa akifuatiliwa kwa karibu sana na kocha wa Super Eagles Stephen Keshi katika kipindi hiki ambapo anaingia katika msimu wa pili na timu yake nchini Uturuki.
Amenukuli Keshi akisema,
"Tutamuhitaji katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia lakini kwasasa ana mambo mengi ya kufanya na klabu yake na tunapaswa kumpa fursa"
No comments:
Post a Comment