Severina Vuckovic anajivunia kuvalia jezi ya Manchester City yenye jina la Edin Dzeko mgongoni.
Dzeko aliifungia Bosnia Ijumaa mchezo wa kufuzu kombe la dunia.
Mshambuliaji Edin Dzeko amekuwa na mashabikiwa wengi sana akiwa na Manchester City baada ya kuibuka kuwa mfungaji mzuri lakini pia kumbe hata barani Ulaya amejijengea heshima kubwa barani humo.
Mshambuliaji huyo alifunga goli katika mchezo baina ya Bosnia and Herzegovina katika mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lichtenstein Ijumaa iliyopita, amewavutia na kuwapagawisha raia wengi wa nchini Croatia.
Nyota wa musiki wa Pop mwanamama Severina Vuckovic ametupia picha akiwa amevalia jezi ya Manchester City ya Dzeko katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram iliyo na saini za mshambuliaji huyo na mgongoni ikiwa na jina la mshambuliaji huyo(tazama picha juu).
Picha hiyo imeonekana kumfurahisha mshambuliaji huyo wa zamani wa Wolfsburg na katika kuonyesha furaha yake ameiweka katika ukurasa wake wa Twitter kwa lengo la kuchangia na mashabiki wake.
Mwanamuziki huyo mwenye kusisimua ambaye ana umri wa miaka 41 ni kipenzi cha mashabiki wa muziki nchini Croatia ambaye kwasasa ameshatoa jumla ya santuri 11 katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Pia aliwahi kuimba wimbo wa nchi hiyo kwa taifa lake wakati wa kuhamasisha ushiriki wa taifa hilo katika michuano ya Ulaya mwaka 2006.
Kwa upande wao Bosnia ambao wanapakana na Croatia wanaweza kufuzu kuelekea katika fainali za kombe la dunia kutoka kungi G endapo watafanikiwa kushinda mchezo wao uliosalia ya hatua ya makundi dhidi ya Lithuania Jumanne ya kesho.
Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufikia hatua hiyo muhimu huku (pinnacle) huku Dzeko akiwa katika ari ya kufanya uzuri na kiwango chake kikiwa juu.
No comments:
Post a Comment