Young Africans kesho watashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam kupamabana na maafande wa jeshi la kujenga Taifa Mgambo
Shooting kutoka mkoani Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara mzunguko wa 11.
Kikosi cha Young Africans mpaka sasa kimejikusanyia jumla ya pointi
19, kikiwa kimecheza michezo 10, kikishinda michezo 5, sare michezo 4 na
kupoteza mchezo mmoja, huku ikiwa ni tofauti ya pointi moja dhidi ya
timu tatu zilizopo juu yake Mbeya City, Azam FC na Simba SC zote zina
pointi 20.
Kocha mkuu wa Yanga amekua akiendelea kukinoa kikosi
chake ambacho kwa sasa kinapigana kuhakikisha kinapata ushindi katika
michezo yake yote mitatu iliyobakia na kuweza kuwa juu kileleni kabla ya
kuanza kwa mzunguko wa pili.
Yanga kesho itashuka dimbani kusaka
pointi tatu muhimu kutoka kwa timu inayoshika mkia Mgambo Shooting na
endapo itaibuka na ushindi katika mchezo inaweza moja kwa moja kukwea
katika nafasi ya kwanza au ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutegemea
na matokeo ya michezo ya leo.
Katika mchezo wa kesho wachezaji
Nizar Khalfani na David Luhende watakosekana kutokana na kuwa majeruhi,
Nizar amechanika nyama za paja (mazoezini) huku Luhende akiendelea na
matibabu kufuatia kupata maumivu ya goti katika mchezo dhidi ya Rhino
Rangers.
Kiungo Haruna Niyonzima pia ataukosa mchezo huo kutokana
na kuomba ruhusa ya siku tatu kwa ajili ya kumaliza matatizo ya
kifamilia yanayomkabali, Niyonzima aliondoka jana kuelekea nchin Rwanda
na anatarajiwa kurudu siku ya jumatano kuungana na wenzake kwa ajili ya
maandalizi ya mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya JKT Ruvu Stars.
Wapenzi,
wanachama na washabiki wa Young Africans mnaombwa kesho kujitokeza kwa
wingi katika dimba la Uwanja wa Taifa kuja kuwashangilia vijana
watakapokua wanaipeperusha bendera ya jangwani dhidi ya Mgambo katika
kusaka pointi tatu muhimu.
No comments:
Post a Comment