Mchezaji wa zamani wa timu ya Ireland kaskazini na
mlinzi wa zamani wa Arsenal Pat Rice amefikishwa hospitalini baada ya
kugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani.
Rice mwenye umri wa miaka 64 aliichezea mara 528
timu ya washika Bunduki wa London pia aliwahi kuwa Kocha msaidizi
akimsaidia Arsene Wenger kwa kipindi cha miaka 16 kabla ya kustaafu
mwaka 2012.
Taarifa ya klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa
Pat yu hospitali akipata matibabu na kumtumia salamu za pole na kumtakia
heri apone haraka.
Rice aliichezea Gunners kwa kipindi cha zaidi ya
misimu 14 baada ya kujiunga na timu ya vijana, ambapo timu yake
ilichukua ubingwa wa Kombe la Ligi na FA mara mbili ,mwaka 1971, pia
alikuwa nahodha wa Timu hiyo ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye
michuano ya FA mwaka 1979.
Wenger amesifu jitihada na kazi ya Rice ambaye alikua akifanya nae kazi mpaka alipostaafu mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment