Fifa imesema haina mpango wa kuhamisha michuano ya
kombe la dunia mwaka 2014 kutoka nchini Brazil ingawa nchi hiyo imepata
changamoto katika maandalizi ya michuano hiyo.
Wafanyakazi wawili walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na nguzo ambazo ziliharibu uwanja wa Corithians ulio mjini Sao Paulo.
Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa
kucheza mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia katika uwanja huo wenye
uwezo wa kuwa na watazamaji 65,000.
Vyanzo vya habari vya juu ndani ya Shirikisho
hilo vimeendelea kusisitiza kuwa hakuna mbadala kutokana na kutokea kwa
ajali hiyo.
Brazil ilikiri kuwa inafanya jitihada za
kumaliza ujenzi wa viwanja 12 kwa ajili ya michuano hiyo, sita kati ya
hivyo ipo tayari kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho.
Ajali iliyotokea siku ya jumatano ni ya tatu
kusababisha kifo katika viwanja vitakavyopigiwa kipute cha kombe la
dunia.Wafanyakazi wengine wawili walipoteza maisha kipindi cha miaka
miwili iliyopita.
Uchunguzi umeanza hii leo kubaini chanzo cha ajali mjini Sao Paulo.
No comments:
Post a Comment