Malky Mackay amefutwa kazi ya umeneja katika klabu ya Cardiff.
Baada ya siku kadhaa za tetesi hatimaye mmiliki wa klabu ya Cardiff, Vincent Tan na bodi ya klabu hiyo imeamua kumuondoa kazini Malky Mackay licha ya licha ya kuonekana kuungwa mkono na mashabiki wa klabu hiyo.
Klabu hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa tweetee imeandika
'The Board of Directors at #CardiffCity have relieved
Malky Mackay of his duties. A new first team manager will be appointed
in due course.'
Malky Mackay amekuzwa kazi baada ya kuwepo na tetesi kwa muda mrefu.
Mmmiliki wa Cardiff Vincent
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 41 raia wa Scotland sasa atalipwa karibu pauni milioni £3.5 kwa ajili ya kufidia kufuzwa kwake kazi.
Mameneja ambao ambao katika nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo ni pamoja na kocha wa zamani England Sven-Goran Eriksson, Mchezaji wa zamani wa Manchester United na meneja wa klabu ya Molde Ole Gunnar Solskjaer na kocha wa kituruki Yilmaz Vural.
Katika hatua nyingine Tan anatarajiwa kukutana na mashabiki wa Cardiff City’ katika mkutano uliopangwa kufanyika Jumamosi.
Kundi maarufu la klabu hiyo linalojulikana kama 'The
Cardiff City Supporters’ Trust' itatuma ujumbe wa watu wanne kukutana na mmiliki saa saba kamili mchana uwanja wa kabla ya mchezo dhidi ya Sunderland.
Kundi hilo lilimpa mmiliki huyo raia wa Malaysia onyo juu ya nini wanataka kufanya ikiwa ni pamoja na kuwa na mazungumzo ambayo yatahusu zaidi juu mtafaruku unaohusu klabu hiyo pamoja na maamuzi ya mmiliki huyo kutaka kubadilisha rangi maalumu ya klabu hiyo na kuwa nyekundu pamoja na kupunguza madeni
Kocha wa zamani wa England Sven Goran Eriksson pichani juu amekuwa akihusishwa na kazi ya umeneja wa Cardiff
Ole Gunnar Solskjaer pia anataka kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment