Pep Guardiola amefanikiwa kujiwekea na kuongeza thamani yake ndani ya Bayern Munich tangu achukue kazi ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo kiangazi ikiwa ni pamoja na mazingira mazima ya kufanyia mazoezi ya kikosi.
Kigogo hicho cha nchini Ujerumani kwasasa kipo mjini Doha kikifanua maandalizi yake kabla ya kurejea katika ngarambe ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya nchini Ujerumani na Guardiaola amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuimarisha kikosi.
Franck Ribery, Mario Mandzukic, Thomas
Muller na Co wamekuwa wakijituma wenyewe ndani ya kituo cha kulelea vipaji cha 'Aspire Academy
for Sports Excellence', wakichanganya mazoezi ya kawaida na kuongeza mbinu nyingine za ziada katika kujiimarisha.
Du! hii si mchezo, nyota wa Bayern wakijiumiza leo kwa faida ya kesho wakiwa ndani ya Doha
Bayern itakuwa ikirejea katika Bundesliga
Januari 24 wakitarajia kuanza dhidi ya Borussia Monchengladbach, wakifuatia na mchezo mwingine siku tano baadaye dhidi ya Stuttgart wakati klabu hiyo ikiwa katika mipango mizito ya kutetea taji lake.
Kikosi cha Guardiola kipo katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani wakiongoza kwa tofauti ya alama saba dhidi ya wanao wafuatia Bayer Leverkusen na wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja.
Ikiwa bado ina michezo mingi ya msimu, na kutokana na dhamira yao ya kweli ya kutwaa kwa mara nyingine tena taji la Bindersliga msimu ujao na mafanikio mengine barani Ulaya na dunia kwa ujumla, tayari klabu hiyo imeshafanikiwa kumsajili Robert Lewandowski kutoka kwa wapinzani wao wakubwa wa ligi ya Bundesliga Borussia Dortmund.
Lewandowski
anasema atajituma kwa moyo wake wote kuisadia Dortmund kabla ya kuelekea Bayern mwishoni mwa msimu.
Pichani: Nifuateni mimi vijana ndivyo anavyoonekana kusema Pep Guardiola akiwa mazoezini kabla ya kurejea katika ngarambe ya ligi kuu ya UJrumani Bundesliga
Wakipasha moto: Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger wakikimbia mazoezini.
Kipa wa Bayern Manuel Neuer akiwa mazoezini akizuia shuti lisiingie nyavuni
Lewandowski,ambaye alisaini kuichezea Bayern Munich kwa mpango wa miaka mitano Jumamosi amewaambia mashabiki wa kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa:
'Bado tuna nusu mwaka mbele yetu ambapo tuna mipango tuliyojiwekea kufanikisha pamoja.
'Hata kama kuna mashabiki wachache miongoni hawakubalini na maamuzi yangu, lakini nategemea uungwaji wenu mkono!'
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameongeza kwa kusema:
'Kwa chochote kitakacho tokea mbele, Nitajitoa kwa ajili ya Borussia Dortmund! mimi bado ni Robert Lewandowski wenu.'
Lewandowski
alijiunga na Dortmund mwaka 2010, na kabla ya kujiunga na Bayern alikuwa mchezaji huru, baada ya kugomea kuongeza mkataba wake wa sasa na Dortmund.
Mario Gotze akifanya vitu kushoto huku upande wa kulia Guardiola akitoa maelekezo
Wakisubiri kucheza: Mitchell Weiser, Daniel Van
Buyten, Jerome Boateng, Rafinha, David Alaba, Javi Martinez na Claudio
Pizarro wakiwa ndani ya uwanja wa mazoezi wa Aspire Academy
No comments:
Post a Comment