KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, January 6, 2014

Baada ya Lewandowski kukamilisha uhamisho huru kwenda Munich, Rockersports inakukumbusha uhamisho nyingine huru 10 (Bosman free transfers) za mafanikio. Bofya zaidi

Robert Lewandowski ataihama Borussia Dortmund na kujiunga na Bayern Munich akiwa huru.


 Robert Lewandowski hatimaye kakamilisha uhamisho huru(Bosman move) kutoka Borussia Dortmund kuelekea Bayern Munich na huwenda akadhihirisha kuwa yeye ndiye usajili bora uliofanyika kwa mwaka huu.
Usajili huu wa mmoja wa washambuliaji bora dunia kutoka kwa vilabu hasimu kisoka nchini UJerumani ambao haukuwa na gharama za uhamisho ni biashara kubwa kufanyika duniani lakini tukumbuke kuwa kumekuwepo pia huko nyuma usajili wa aina hii ambapo nyota walihama kutoka katika klabu moja kubwa na kuelekea katika klabu nyingine kubwa bila kugharimu ada za uhamisho.

Kutoka kwa Roberto Baggio mpaka kwa Campbell na mpaka kufika kwa Pirlo, Rockersports inakukumbusha wale kumi waliotikisa lakini wakihama huru(Top 10 Bosman transfers).

STEVE McMANAMAN

McManaman alisaini mkataba wa miaka mitano na Real Madrid mwaka 1999, baada ya kugomea utashi wa kuongeza mkataba wa klabu ya Liverpool na ofa nyingine mbalimbali kutoka katika vilabu kama Barcelona, Lazio, Inter Milan na Juventus.
Aliondosha maoni ya wakati huo akiwa England kuwa yeye ni winga na alipotua tu Hispania alidhihirisha kuwa kuwa yeye ni kiungo wa ushindani, ambako aligeuka kuwa mchezaji muhimu (yaani key player) akiwa Real na kufanikisha kupata mataji mawili ya La Liga,European Super Cup, kombe la dunia na mataji mawili ya Champions Leagues.
Champions League winner: Steve McManaman proved a big success at Real Madrid after leaving Liverpool
Steve McManaman alidhihirisha ubora wake alipokuwa na Real Madrid baada ya kuihama Liverpool

THE BOSMAN RULING

Hii ni sheria ya umoja wa Ulaya' EU' ambayo inaruhusu mchezaji anapokuwa nje ya mkataba kuondoka katika klabu zao bila klabu aliyokuwa akiichezea kupata ada ya uhamisho.

Ilipewa jina baada ya mshambuliaji wa Belgian Jean-Marc Bosman, ambaye aliipeleka klabu yake ya, RC Liege mahakamani akitaka kuihama na kujiunga na Dunkerque tofauti na mwajiri wake alivyokuwa anataka.

Mwaka 1995, mahakama ya Ulaya 'European Court of Justice' iliondoa kizuwizi hicho kwa wachezaji wa kigeni ndani ya Ulaya wakiwa katika ligi za nchi mbalimbali, na hivyo kuruhusu wachezaji ndani ya EU kuhamia vilabu vingine mwishoni mwa msimu bila ya ada ya uhamisho kulipwa.

HENRIK LARSSON

Henrik Larsson aliitumikia Barcelona kwa miaka miwili baada ya kuihama Celtic mwaka 2004 alikuwa alikuja kupata mafanikio alipokuwa huko, kwani alishinda mataji mawili ya La Liga, Spanish Super Cup na  Champions League.

Kuwasili kwa Samuel Eto'o na baada ya kupata jeraha la msuli, ndio ilikuwa tatizo kwa raia huyo wa Sweden kuonekana tena lakini bado amekuwa akipewa sifa zake kwa kufanikisha taji la ligi ya mabingwa Ulaya ambalo Barca ilitwaa mwaka 2006 ilipoishinda Arsenal katika fainali ambapo yeye aliingia akitokea benchi wakiwa nyuma kwa bao 1-0 alikuwa kivutio.

'Aliuubadilisha mchezo,' alikaririwa Thierry Henry akisema hivyo baada ya mchezo.
Nukuu ya Henri iliendelea kusomeka
 'yeye ndiye aliua mchezo– wakati mwingine unamzungumzia mtu kama Ronaldinho na Eto'o lakini pia unatakiwa kuzungumzia watu bora kama hawa, wanaingia na kuleta tofauti na huyu si mwingine alikuwa ni Henrik Larsson tonight.'
Decorated: Henrik Larsson was among the shrewdest signings in recent years when he joined Barcelona
Ali-Decorate mchezo: Henrik Larsson alikuwa ni mmoja wa usajili huru alipojiunga na Barcelona

MICHAEL BALLACK

Real Madrid na Manchester United zote zilionyesha nia kwa Michael Ballack mwaka 2006 lakini aliamua kujiunga na Chelsea.
Majeraha ya enka yalizima mafanikio yake katika msimu wa kwanza wa kuhama kwake lakini mwaka uliofuata 2007-2008, wakati Chelsea ikifikia fainali ya ligi ya mabingwa na wakipambana na Manchester United, Ballack alikuwa mchezaji bora na alijiimarisha zaidi na kuwa mmoja wa wachezaji bora wanaochezea ligi kuu ya England 'Premier League' mpaka alipoondoka London mwaka 2010.
Commanding figure: Michael Ballack rejected some of Europe's biggest teams to join Chelsea in 2006
Michael Ballack aligomea ofa za vilabu mbalimbali Ulaya na kujiunga akiwa huru na Chelsea mwaka 2006

SOL CAMPBELL

Kwa mashabiki wa Tottenham, Sol Campbell siku zote wataendelea kulikumbuka jina la 'Judas' ambalo walimpachika baada ya kuwahama wapinzani wao wakubwa Arsenal mwaka 2001. 
Uhamisho wake uliokumbwa na maneno mengi hatimaye ulikuja kumpa mafanikio.
Baadaye alikuja kushinda mataji mawili ya 'Premier League', taji moja la FA Cup na kucheza katika fainali ya ligi ya mabingwa, mafanikio ambayo asingeweza kuyapata endapo kama angejiunga na Spurs iliyokuwa ikimtaka, ambapo alikuja kuwa muhimu sana katika kikosi cha Arsenal ambacho kilijulikana kama 'undefeated' msimu wa mwaka 2003-2004 ndani ya Premier League.
Portsmouth pia ilifaidika kwani baadaye Campbell aliondoaka Arsenal akiwa huru mwaka 2006.
Controversial: Sol Campbell shocked the football world when he left Tottenham for Arsenal in 2001
Sol Campbell aliikacha Tottenham na kujiunga na Arsenal akiwa mchezaji huru mwaka 2001

MARKUS BABBEL

Babbel akijunga na Liverpool akitokea Bayern Munich na kuonekana kama mmoja wa walinzi wa kushoto bora barani Ulaya licha ya msimu wa kwanza wa 2000-2001, kuwa katika majeraha lakini msimu uliofuata alikuwa bora ndani ya Premier League.
Liverpool lishinda taji la FA, UEFA Cup na League Cup na Babbel alikuja kuwa muhimu kama ilivyokuwa kwa wengine akina Sami Hyypia katika sehemu ya Ulinzi.
Consistent performer: Markus Babbel (left) excelled as Liverpool won a cup treble in 2001
Markus Babbel

FERNANDO LLORENTE

Kama ilivyo kwa Lewandowski, Llorente alikuwa ni mmoja wa washambuliaji wazuri barani Ulaya ambapo alikubali kujiunga na Juventus akitokea Athletic Bilbao msimu uliopita.

Nyota huyo raia wa Hispania alipigana kudhihirisha ubora wake lakini na hivi karibuni amekaribia kwenye ubora wakiwa sambamba na Carlos Tevez ambapo wamefanikiwa kutengeneza moja ya safu bora za ushambuliaji barani Ulaya. Kwasasa yuko katika mkataba wa miaka mitatu na kigogo hicho cha Turin na anakaribia kushinda taji huku akifunga mabao.
Class act: Juventus' Fernando Llorente became one of Europe's best strikers at Athletic Bilbao
Fernando Llorente amekuwa ni mmoja ya washambuliaji bora Ulaya

BRAD FRIEDEL

Liverpool alimruhusu Friedel kuondoka akiwa huru mwaka 2000, huku Sander Westerveld akiwa ndio chaguo la kwanza, halikuwa wazo baya kipindi kile ambapo baadaye lilionekana kuwa lilikuwa ni kosa kubwa.
Blackburn hatimaye ikafaidika na mlinda mlango huyo ambaye hakukosekana katika mchezo hata mmoja ambapo alicheza michezo 287(hata kuweza kuifungia mara moja) mpaka alipojiunga na Aston Villa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £2.5 mwaka 2008. Hivi karibuni amekuwa ni mlinda mlango chaguo la kwanza katika kikosi cha Tottenham na anaendelea kuwa hivyo ingawa umri wake unaingia katika miaka 40Model professional: Brad Friedel established himself as a quality Premier League goalkeeper at Blackburn
Brad Friedel

ESTEBAN CAMBIASSO

Cambiasso hakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid licha ya Claude Makelele kuondoka na akajiunga na Inter Milan kwa uhamisho huru mwaka 2004.
Ameendelea kuichezea klabu hiyo mpaka kufikisha jumla ya michezo 400 na kuendelea kuwa tegemeo ambapo walishinda taji la mwaka 2010, chini ya Jose Mourinho. Pia aliendelea kushinda mataji mengine manne.
Treble winner: It was a mistake by Real Madrid to allow Esteban Cambiasso to leave for Inter Milan
Lilikuwa kosa kwa Real Madrid kumruhusu Esteban Cambiasso na kujiunga na Inter Milan

ROBERTO BAGGIO

Kipindi cha ucheza cha Roberto Baggio kilikuwa ni cha kupanda na kushuka, hivyo alikuja baadaye kupata mafanikio akiwa Bologna baadaye kufuatia mwaka 1997 kuondoaka AC Milan. 

Akiachwa na Arrigo Sacchi ndani ya San Siro, Baggio alikuja kuwa tegemeo kwa Bologna, ambapo alikisaidia kikosi hicho kilichokuwa katika hali mbaya na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Serie A, ahsante kwa magoli yake 22.
 
Aliendelea kucheza soka la mvuto kiasi kuushawishi uma katika kikosi cha Italia katika kombe la dunia mwaka 1998 na baadaye kujiunga na Inter.
Colossal figure: Roberto Baggio impressively rebuilt his career at Bologna after leaving AC Milan
Roberto Baggio

ANDREA PIRLO

Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wakujivunia, na haikuwa kazi kubwa kumtabiria Pirlo kuwa alikuwa akielekea mwishoni wakati akiondoaka AC Milan na kujiunga na Juventus mwaka 2011.
Badala yake alijiimarisha na kuwa mmoja kati ya viungo hatari barani Ulaya wakati Juventus kwa mara nyingine tena ilipoibuka kuwa timu bora nchini Italia na Milan ilipo poromoka kwa haraka.
Pirlo pia alikuja kuwa kivutio katika kikosi cha Italy katika fainali za Euro 2012 na amekuwa ni mtaliano pekee kuteuliwa katika kinyang'any'iro cha tuzo ya Ballon d'Or 2013.
Evergreen: Juventus' Andrea Pirlo is still considered one of Europe's best midfielders
Andrea Pirlo bado anatazamwa kama mmoja wa viungo bora Ulaya.

No comments:

Post a Comment