Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Taifa Uganda na klabu ya Young
Africans Emmanuel Arnold Okwi leo ameruhiswa ramsi kuanza kuitumikia
timu yake katika michezo ya Ligi Kuu na Mashindano ya klabu Bingwa
Barani Afrika kufuatia shirikisho la soka nchini TFF kuiandikia barua
klabu ya Young Africans.
Okwi ambaye alisajiliw aa Young Africans mwishoni mwa mwaka jana na
kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, alisimamishwa na
Shirikisho la Soka la Nchini TFF wakati wakisubiria kupata udhibitisho
wa usajili wake kutoka FIFA.
Mara baada ya barua hiyo, Okwi
anatarajiwa kuungana na wenzake mwishoni mwa wiki mara timu itakaporejea
kutoka Visiwa vya Comoro na ataanza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting siku ya jumamosi Februari 22 mwaka
huu.
Uongozi wa Young Africans
unawashukuru wanachama, wapenzi na wadau kwa ujumla kwa kuwa wavumilivu
wakati wa suala na hili na hatimaye limepatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment