Raja Casablanca imeanza kampeni ya vilabu bingwa Afrika kwa ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Diamond Stars ya Sierra Leone.
Mabingwa hao wa Morocco ambao walichapwa bao 2-0 na mabingwa wa Ulaya Bayern Minich katika michuani ya vilabu bingwa dunia mwezi desemba walipata mabao yao kupitia kwa Mouhssine Iajour aliyefunga mabao manne, huku magoli mengine yakifungwa na Abdelilah Hafidi na Abdelkabir El Ouadi.
Klabu bingwa ya Libya Al Ahly Benghazi
pia wameanza vema kampeni ya vilabu katika mzunguko wa kwanza kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Foullah Edifice
ya Chad mchezo uliopigwa mjini Tunis.
Licha ya kucheza ugenini kutoka na hali ya usalama nchini Libya Ahly walitawala mchezo wakimtumia zaidi nyota wa kimataifa wa Zimbabwe Edward Sadomba ambaye alifunga magoli mawili.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Dynamos aliandika bao la kwanza kunako dakika ya 26
kabla ya Abdelrahman Fetori kuandika la pili kwa mkwaju wa penati baada ya mapumziko.
Moataz Al Mehdi aliandika bao la tatu kunako dakika ya 71 ya mchezo kabla ya Sadomba kukamilisha karamu hiyo ya mabao dakika moja kabla ya mchezo kumalizika.
Kaizer Chiefs hii leo wako dimbani dhidi ya
Black Africa
kutoka Namibia.
Zamalek wanaumana dhidi ya AS Douanes
ya Niger, Enyimba wakikabiliana dhidi ya Ange de Notse
ya Togo huku Kotoko wakikapambana dhidi ya Barrack Young Controllers
ya Liberia.
No comments:
Post a Comment