KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 5, 2014

Bayer Leverkusen yamfuta kazi Sami Hyypia kufuatia ushindi wa mchezo mmoja katika jumla ya michezo 12.


Bayer Leverkusen amemfuta kazi kocha wake mkuu Sami Hyypia kufuatia kupata ushindi katika mchezo mmoja tu miongoni mwa michezo 12 iliyopita.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni mlinzi wa zamani wa Liverpool alikuwa kocha pekee wa klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu ambapo hapo kabla alikuwa akifanya kazi na Sascha Lewandowski.
Lewandowski mwenye umri wa miaka 42, ambaye aliwahi aliwahi kufanya kazi katika katika timu za vijana aliingia mpaka kumalizika kwa msimu.
Leverkusen ilipoteza mchezo kwa kufungwa magoli 2-1 dhidi ya Hamburg hapo jana Ijumaa kiasi kuweka matumaini ya klabu hiyo kutinga katika michuano ya klabu bingwa mashakani.
Sami Hyypia Champions League trophy
Hyypia alishinda ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2005
Wanasali katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundersliga huku Wolfsburg, Borussia Dotmund, Monchengladbach na Mainz wakiwa mbele yao na wote wakiwa na mchezo mmoja wa ziada.
Taarifa ya klabu hiyo imesomeka ikisema
"Matokeo ya michezo yetu ya hivi karibuni yamekuweka katika ya kutokuwa na maamuzi mengine " Amenukuliwa mkurugenzi wa michezo Rudi Voller, ambaye ni nyota wa zamani wa Ujerumani.

Alijiunga Leverkusen kama mchezaji mwaka  2009 kabla ya kustaafu miaka miwili baadaye, Hyypia aliteuliwa katika jopo la makocha sambamba na Lewandowski mwezi April 2012. 
Liverkusen ikiongozwa na Hippia alitinga ligi ya mabingwa msimu uliopita licha ya baadaye kuchapwa bao 5-0 katika uwanja wake wa nyumbani na Manchester United, hata hiyo ilitinga tena katika hatua ya timu 16 bora kabla ya kupoteza nafasi ya kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 6-1 kwa ushindi wa jumla dhidi ya Paris-St Germain.

Hyypia, ambaye aliichezea timu ya taifa ya nchi yake ya Finland jumla ya michezo 105 alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliofanikisha ushindi wa taji la ligi ya mabingwa akiwa katika kikosi cha Liverpool mnamo mwaka 2005, na pia alikuwa ni sehemu ya wachezaji waliotengeza historia ya kuchukua mataji ya FA Cup, League Cup na Uefa Cup mwaka 2001.

Alisajili wa na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £2.5 kutoka katika klabu ya Willem II ya Uholanzi mwaka 1999, na kuichezea michezo 464 katika muongo mzima ndani ya Anfield.

No comments:

Post a Comment