Mtu mmoja mvamizi wa uwanja akionekana kumchanganya kila mmoja aliyemshuhudia aliingia uwanjani akiwa amevalia jezi ya Real Madrid katika mchezo wa kirafiki ambao Madrid walipoteza kwa Fiorentina kwa bao 2-1 hapo jana.
Shabiki huyo alionekana akikimbilia katikati ya uwanja wa Warsaw akiwa amevalia jezi iliyokuwa na namba 7 mgongoni ikiwa na jina la Cristiano Ronaldo kabla ya jaribio lake la kutaka kujichanganya.
Baada ya kufanikiwa kuzungumza kidogo na Karim Benzema uwanjani, watu wa usalama wa usalama wakaingia uwanjani na kumsindikiza mpaka nje kabla ya kupata faraja ya Ronaldo aliyeifungia mabingwa hao wa Ulaya bao kunako dakika ya nne.
Tukio hilo limekuja saa nne kabla ya shabiki mwingine kuarifiwa kuingia uwanjani umbali wa yadi 70 uwanja wa Boleyn wakati Westham walipowazamisha Tottenham Hotspur ambapo alifanikiwa kuupiga mpira kabla ya kukimbilia nje.
No comments:
Post a Comment