Inaarifiwa kuwa Juventus wako mbioni sambamba na Liverpool kumnasa mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao kiangazi hii.
Kigogo hicho cha Turin kimekuwa kikimuhitaji sana mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia kwa lengo la kuziba pengo la Fernando Llorente, ambaye huenda akaondoka Turin na kuelekea
Valencia, hizi zikiwa ni taarifa kupitia gazeti la Kitaliano la 'La Gazzetta Sportiva'.
Falcao amekuwa akihusishwa na kuelekea Real Madrid na Liverpool
kwa mkopo katika siku za hivi karibuni na amekuwa akikaribia kabisa na kujiunga Santiago Bernabeu.
Hata hivyo kumekuwe na taarifa kuwa kocha wa Los Blancos Carlo Ancelotti ametupilia mbali mpango huo pale alipothibitisha kuwa kigogo hicho cha Hispania hakitaongeza tena mchezaji kingazi hii huku Juve wakionekana wakiendelea na harakati hizo.
No comments:
Post a Comment