Uchaguzi wa goli lipi litalikuwa bora katika msimu mpya wa 'Premier League' kwasasa itakuwa ni mapema kusema lolote lakini Jordan Henderson tayari amejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza mpira mzuri wa mwisho uliozaa goli.
Kiungo huyo alitoa pasi murua kwa Raheem Sterling aliyeandika bao la kwanza kwa Liverpool dhidi ya Southampton mchana wa leo.
Inaweza ikatokea mipira mizuri ya kupenyeza ya mwisho hapo baadaye kiasi cha miezi tisa ijayo, lakini juhudi za Henderson zimeandikisha ushindani wa mpira bora wa mwisho katika michezo mingine ijayo.
Mchezo wenyewe ulivyokuwa
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alikuwa na kila sababu ya kutabasamu alipoingia uwanjani Anfield na kuwasikia mashabiki wa klabu hiyo wakishangilia na kuimba nyimbo za kumsifu kwa kuiokoa klabu hiyo msimu uliopita alipoiongoza kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City.
Lakini wapinzani wao Southampton licha ya kuwa walikuwa wamewapoteza wachezaji watatu kwa mahasimu wao Liverpool hawakuwa wepesi wa kupisha mpira .
Liverpool nayo ilikuwa na kibarua cha kujaza pengo lililowachwa wazi na mfungaji mabao mengi msimu uliyopita katika ligi kuu ya Uingereza Luis Suarez.
Mfungaji bao la Liverpool Raheem Sterling |
The reds ndio walioonesha tamaa ya kutaka ushindi na labda kuendeleza msururu wa matokeo mema msimu uliopita.
Juhudi zao zilizaa matunda kunako dakika ya 23 chipukizi Raheem Sterling alipofuma kimiani bao la ufunguzi dhidi ya the saints.
Baada ya nipe nikupe kati ya timu hizo mbili ,mfungaji bao la kwanza Sterling alirejea nyuma katika badiliko la mfumo baada ya kuonekana kuwa safu ya kati ilikuwa imelemazwa na the saints waliokuwa wakiongozwa na Mugabe Wanyama.
Mabadiliko hayo yalimfaa Brendan ambaye alimuingiza Rickie Lambert.
Lambert alichukua nafasi ya Philippe Coutinho ambaye alikuwa amekwisha cheza kwa dakika 75,
Badiliko hilo lilizaa matunda papo hapo Daniel Sturridge alipoifungia Liverpool kunako dakika ya 79 ya kipindi cha pili na kuirejeshea the Reds uongozi wa mechi hiyo.
Hayo yote ni kenda, Liverpool wamepata ushindi wa 2-1 na kujizolea alama tatu muhimu dhidi ya Southampton katika mechi yao ya kwanza ya ligi kuu msimu huu bila ya mshambulizi wao wa kutegemewa Suarez.
No comments:
Post a Comment