Hernandez kwasasa ni mshambuliaji wa Real Madrid baada ya United kuthibtisha mchana wa leo |
Javier
Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid huku tayari kukiwa na uwezekano mkubwa wa kusalia katika klabu hiyo mpya kwa minajili ya mkataba wa kudumu msimu ujao.
United
imetaka kiasi cha pauni milioni £17 endapo wa kusalia Madrid moja kwa moja utafikiwa lakini makubaliano ya kuelekea huko kwa mkopo yamefikiwa ambapo meneja Louis van Gaal atakuwa amepokea kiasi cha pauni milioni £1.5 malipo ya mshambuliaji huyo hana nafasi kwasasa.
United imethibitisha mpango huo kupitia ukurasa wao wa twitter mchana wa leo.
Dole: Hernandez akitabasamu ndani ya chumba cha vikombe mbalimbali Bernabeu
Yuko sawa kucheza: Hernandez akiwa katika picha wakati wa kupima afya kabla ya kujiunga na Real Madrid
Mpango umekamilika: Mshambuliaji wa Manchester United akisaini jezi za mashabiki nje ya kituo cha kupima afya huko Madrid
Picha za kujipiga: Hernandez akichukua fursa kupiga picha na mashabiki
No comments:
Post a Comment