Kazini Ujerumani: Shinji Kagawa ndani ya jezi ya mazoezi ya Dortmund |
Shinji
Kagawa alikuwa ni kama anarejea nyumbani akiwa katika hali yha kawaida alipowasili Borussia Dortmund akitokea Manchester United ambapo alipata mapokezi makubwa kutoka kwa meneja Jurgen Klopp.
Kagawa mwenye umri wa miaka 25 ameungana tena na klabu yake hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ujrrumani maarufu kama Bundesliga kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni £6.3 ikiwa ni miaka miwili tangu kuihama na kujiunga na United.
Kagawa amesaini mkataba wa miaka minne ambapo Dortmund wao walimuuza kiungo huyo kwa United kwa pauni milioni £12 kwaka 2012.
Kagawa akipiga tizi ni kama hakuna kilicho badilika
Kagawa akipiga tizi kwa usimamizi wa daktari wa timu Andreas Schlumberger
Narejea nyumani: Borussia Dortmund imesainisha kiungo Shinji Kagawa kutoka Manchester United kwa dau la pauni milioni £6.3
Karibu Nyumbani Dortmund Kagawa akikutana na meneja Klopp
Majeraha yalidumaza maendeleo ya kiungo huyo na kushindwa kuwa vizuri chini ya David Moyes na kuonekana hana nafasi chini ya Louis van Gaal.
No comments:
Post a Comment