KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 3, 2010

Hispania na ureno zaelekea kupata nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 Hispania na Ureno kwa pamoja zimezumbua aina nyingine ya kulivutia shirikisho la kandanda duniani kutokana na kuvutia kwa viwanja ambavyo vitatumika katika fainali ya kombe la dunia na hivyo kutengeneza nafasi kubwa ya kushinda tenda ya maandalizi ya kombe la dunia
Kiwanja cha klabu ya Real Madrid cha Bernabeu ndicho kiwanja kilicho tumika katika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwama huu wa 2010
Mataifa hayo mawili kwa pamoja yamekuwa ni miongoni mwa mataifa ambayo yana uzoefu mkubwa wa maandalizi ya fainali kubwa lakini mara hii katika kujaribu kulivutia shirikisho la kandanda dunia fifa yameamua kuungana kuwania nafasi ya kuandaa fainali ya kombe la dunia kwa miaka ya 2018 ama 2022 ambapo kwa sasa FIFA kupitia kamati yake ya uchunguzi imeenza kampeni ya kuchunguza ubora wa maandalizi hayo
Hispania na Ureno ni miongoni tu mwa mataifa kadhaa ambayo yamependekeza kwa fifa kuandaa fainali hizo katika miaka hiyo ikiwa ni pamoja na uingereza huku mkaguzi mkuu wa fifa Harold Mayne-Nicholls akisema mataifa hayo katika ripoti yao yameonekana kuvutia zaidi baada ya kukamilisha uchunguzi wao wa siku nne.
Mataifa mengine ni pamoja na Urusi, Uingereza, Marekani ubelgiji kwa pamoja na Uholanzi Hispania na Ureno.
Mataifa ya Japan,Australia,Qatar na Korea Kusini wenyewe wamejipanga kwa ajili ya kuandaa fainali za mwaka 2022
Juma lijalo wakaguzi wa FIFA wataelekea nchini Mrekani kwa ukaguzi katika nchi hiyo kabla ya kumalizia nchini Qatar kabla ya kamati ya utendaji ya FIFA kutoa maamuzi yake December 2.

SNEIJDER ATAZAMA MAFANIKIO MENGINE BAADA YA KOMBE LA DUNIA SAFARI EURO 2012Kuelekea katika mchezo wa leo wa kuwania kufuzu kwa ajili ya fainali za mataifa ya ulaya dhidi ya San Marino mchezo ambao utapigwa katika dimba la Olimpico Serravalle usiku wa leo nyota aliyengara katika fainali za kombe la dunia Wesley Sneijder ameonekana kuyatazama mafanikio ya uholanzi katika fainali hizo kama kioo cha timu hiyo kufanya vizuri katika kampeni za kufuzu ulaya
Katika fainli za kombe la dunia nchini Afrika kusini uholanzi maarufu kama Oranje ilifanikiwa kufika katika hatua ya fainali na kutolewa na Hispania kwa bao 1-0 bao la Iniesta

Akikaririwa anasema
"kiukweli kama natazama picha huko nyuma nakumbuka great moments,Because we did have great moments. And yes we had a bad result in the final, but to get there with our team, with the qualities we had, with the small country we come from, it's a big thing."
Wakati hayo yakiwa hivyo kocha wa wadutch hao Bert Van Marwijk amezungumzia juu ya maamuzi yake ya kumteua kiungo wa Bayern Munich Mark van Bommel kama nahodha baada ya kutangaza kujiuzulu kwa nahodha wa zamni Giovanni van Bronckhorst.
Anasema Jambo la kwanza ni muaminifu kwake "He is a good organiser on the pitch.
"nafasi yake kiwanjani pia muhimu kwa kuwa nahodha wa kikosi na amesha wahi kuwa nahodha wa Bayern na PSV. Anyway chaguo hili kwake linakubalika na ana umri mzuri."

DAVID BECKHAM ANAJIPANGA KUREJEA GALAXY KIMYA KIMYA David Beckham anatarajia kurejea mapema tofauti na ilivyo tegemewa katika klabu yake ya Los Angeles Galaxy kunako September 11.
Kiungo huyo wa uingereza mwenye umri wa miaka 35 hajaonekana katika mchezo wowote mgumu na wakiushindani tangu aumie kifundo cha mguu akiitumikia AC Milan mwezi March,maumivu ambayo yalimaliza matumaini yake ya kuichezea uingereza katika fainali ya nne ya kombe la dunia huko chini Afrika kusini.




Amekuwa katika program maalum ya ukarabati na sasa baada ya hali kuonekana kuanza kutengemaa katika afya yake sasa anakabiliwa na mchezo wa Mojor League Soccer dhidi ya Columbus.
Beckham anarejea katika mazoezi huko Galaxy August 11 badala ya tangazo lake la awali la kujuzulu.

No comments:

Post a Comment