KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 1, 2010

MAVUVUZELA MARUFUKU ULAYA UEFA YASEMA SI UTAMADUNI WA ULAYA
The vuvuzela pia yakitambulika kama lepatata katika lugha ya Tswana yakiwa mara nyingi na urefu wa sentimeta 65 (au futi 2 katika material ya plastic
UEFA imepiga marufuku matumizi ya vuvuzela katika michuano ya yote ya ulaya ikiwa ni pamoja na michuano ya Champions League, Europa League na michuano ya kufuzu Euro 2012.
Itakumbukwa kuwa vuvuzelas imekuwa katika hali ya kukosolewa katika katika fainali za kombe la dunia 2010 kiasi kuarifiwa kuwa yamekuwa na kelele na kutazamwa kwa namna ya aina yake kama yaruhusiwe huko ulaya ama laa.
Katika hatua nyingine UEFA imetaka mashabiki wasibebe mavuvuzela kuelekea viwanjani kwa kuwa hayatakuwa na nafasi kutumika katika michuano mbalimbali barani ulaya.
Kwa mujibi wa taarifa iliyotolewa na EUFA imesomeka
"bodi ya utawala ya kandanda la ulaya imewajulisha wanachama wake 53 kuwa maamuzi hayo ni kutokana na misingi ya utamaduni ya soka la ulaya huku pia wakisema mazingira katika michezo inawezekana kubadilika kutokana na matumizi ya Vuvuzela" .




MILAN YAKAMILISHA USAJILI WA ROBINHO TOKA MANCHESTER CITYMilan yakamilisha usajili wa Robinho toka Manchester City
Robinho amejiunga na Milan kumaliza mzozo mkubwa baada ya kuwa katika tetesi baada ya kumaliza mkopo katika klabu ya Santos.
Milan imekamilisha usajili wa Robinho toka Manchester City kwa mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Serie ikithibitsha hilo kupitia mtandao wa klabu yao hapo jana.
Taarifa iliyosomeka kupitia mtandao wa klabu hiyo inasomeka
"AC Milan inatoa taarifa kuwa imefanikiwa kumdaka Robinho toka Manchester City. Nyota huyo wa Brazil amesaini mkataba wa miaka minne "imesomeka taarifa hiyo
Amefanikisha vipimo vya afya huko Rossoneri na atakuwa akilipwa euro milioni €18 million jumlisha na bonuses nyingine mbalimbali licha ya kwamba ada ya uhamisho haikuwekwa wazi wakati wa tangazo rasmi lilipotoka .

Sasa anaungana na nyota kadha wakali kama mwenzake kiungo Ronaldinho, Zlatan Ibrahimovic na Alexandre Pato kutengeneza makali katika sehem ya ushambuliaji hususani katika kipindi hiki cha msimu wa michuano ya vilabu ulaya


Van der Vaart afurahia kuelekea Totternham SpursVan der Vaart afurahia kuelekea Spurs
Tottenham Hotspur bado wanaendelea kusikilizia kama watapata huduma toka kwa mshambuliaji ya Rafael van der Vaart lakini mdutch huyo wakati huu ambapo amearifiwa kutaka kujunga na klabu yake huyo mpya. Rafael van der Vaart tayari amearifiwa kutolewa posa ya EURO milioni €11 na klabu ya Tottenham huku kwasasa mpango huo ukiendela kusubiriwa kuthibitishwa
Bosi wa Spurs Harry Redknapp amekuwa katika mkao wa kula akimrubiria Van der Vaart tangu jana mchana huku tatizo kubwa likionekana kuwa ni “personal terms” na kiungo huyo wa Real Madrid
Imearifiwa kuwa uongozi wa Premier League umeelewa tatizo ambalo limeelezwa na Spurs na wakijaribu kuchunguza tatizo hilo ambalo limeelezewa kuwa ni ugumu wa kiteknolojia kufuatia “computer servers”zilizo tumika kuandika taarifa na kusukuma taarifa kati ya vilabu hivyo viwili yaani Spurs na Real kushindwa kudsafirisha documents muhimu kwa wakati . hata hivyo klabu hiyo imeomba suala lao kuangaliwa kwa namna ya kipekee ili kukamilishwa kama lilivyo kusudiwa.

Katika hatua nyingine Van der Vaart tayari ameshazungumzia kufurahishwa kwake na mpango wa uhamisho wake wenye thamani ya euro milioni €11 kwa mkataba wa miaka minne na yuko tayari kujipima na changamoto ya Premier League.katika taarifa zilizo ingia hivi punde kupiti mtandao wa Goal.com “ BREAKING NEWS” zinasema hatimaye Tottenham Hotspur imekamilisha usajili wa Rafael van der Vaart kutoka Real Madrid huku taarifa zaidi zikisema taarifa zaidi zitafuata.




MOHAMED ZIDAN AREJEA UJERUMANI BAADA YA MAJERUHIKufuatia kuwa katika majeraha ya muda mrefu yaliyomuweka nje ya uwanja ikiwa ni pamoja na michezo kadhaa ya kimataifa ya hatimaye mshambuliaji Mohamed Zidan anatarajia kurejea dimbani katika klabu yake ya Dortmund juma hili.
Mshambuliaji huyo wa Misri Zidan atarejea katika klabu yake ya Borussia Dortmund juma hili ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa klabu yake.Zidan mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akisumbuliwa na msuli mkubwa tangu mwezi April na katika kipindi chote alichokuwa katika kurejesha afya yake alikuwa katika kazi yake ya awali ya jeshi la Misri .
Akikaririwa kupitia mtandao wa klabu yake amesema maumivu yake yanaendelea uzuri.Kufuatia kurejea kwake katika nchini ujerumani mshambuliaji huyo wa zamani wa Hamburg atalazimika kukutana na daktari wa klabu yake ya Dortmund Markus Braun ambaye atakuwa na wajibu wa kusema ni kwa kipindi gani mchezaji huyo atarejea rasmi dimbani

No comments:

Post a Comment