KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 20, 2010


LIONEL MESS AKUMBWA NA BALAA, SASA KUSUBIRI KWA WIKI MBILI Hali ya nyota wa Barcelona Lionel Messi imeingia katika utata kufuatia kukumbana na matatizo yanayoaminika kuwa ni ankle ambayo yametokana na na mchezo ambao Barcelona walikuwa dimbani dhidi ya Atletico Madrid katika ligi kuu ya hispnia maarufu kama La Liga ambapo Barca wameibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alilazimika kubebwa katika machela na kutolewa nje katika dakika za majeruhi baada ya tackling toka kwa mlinzi wa Atletico Tomas Ujfalusi na huenda sasa akawa nje ya dimba kwa takribani wiki mbili.

Taarifa ya klabu ya Barcelona kupitia mtandao imethibitisha kuwa Messi ameumia katika mshipa wa wa ankle katika mguu wa kulia.

Mchezaji huyo bora wa dunia wa mwaka huu anatarajiwa sasa kufanyiwa vipimo hii leo jumatatu kuangaliwa ukubwa wa majeraha yenyewe.


Licha ya mlinzi Ujfalusi kukabidhiwa kadi ya pili ya njano kwa tukio hilo lakini bado kocha wa Barcelona Pep Guardiola amemlalamikia mwamuzi wa mchezo huo David Fernández Borbalán.

Anasema "ni kweli tumeshinda mchezo lakini tunasikitishwa na Messi,"

Anasema “si tu Cristiano Ronaldo anaye hitaji ulinzi mwamuzi napaswa kulinda wachezaji wote."

Messi sasa huenda atakosekana katika michezo ya ligi dhidi ya Sporting Gijon, Real Mallorca na Athletic Bilbao pamoja na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rubin Kazan September 29.

Katika mchezo huo Messi alifunga bao la kuongoza la Barcelona katika dakika ya 13 mchezo ambao umepigwa katika dimba la Vicente Calderon Stadium,kabla ya Raul Garcia kusawazisha dakika 11 baadaye na bao la pili kuwekwa kimiani na Gerard Pique



LIVEPOOL YAKAMULIWA NA MASHETANI WEKUNDU OLD TRAFFORD PREMIER LEAGUE ROUND-UP
Berbatov angara katika ushindi wa United ilhali The Blues wakiendeleza ubabe wao

Mabao matatu ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo yaani “hat trick” ya Dimitar Berbatov yanaiwezesha Manchester United kupata ushindi mnono wa mbao 3-2 dhidi ya Liverpool huku mabao ya Liverpool yakiwekwa kimiani na Steven Gerrard

Hata hivyo Chelsea imeendelea kusalia katika usukani wa ligi hiyo baada ya kuikamua Blackpool kwa jumla ya mabao 4-0.

Mabao ya Chelsea yakiwekwa kimiani na Salomon Kalou, florent Malouda akikamua mara mbili huku Didier Drogba akipeleka kimiani mara moja

Mchezo mwingine Manchester City wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 huku mabao yakiwekwa kimiani na Yaya Toure ambaye amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika mchezo uliopigwa katika dimba DW na huku bao lingine ambalo lilikuwa la kwanza likifungwa na Carlos Tevez

No comments:

Post a Comment