KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 20, 2010

MWISHO MWAMPAMBA TUMBO JOTO KWA UTI ANAMTENGENEZEA ZENGWE LA CHUKI KWA MADEMU, UTI ANASHTUKIA MCHEZO KAZI IMEANZA KUELEKEA MWISHO WA SHINDANO Uti anasema Mwisho Mwampamba anamhofia sana kufuatia kuonekana kuwa na umri mzuri na wanawake wanamuheshimu .

Katika kile kinachonekana kuwa kama kuanza kuogopana katika kazungumzo ya chini kwa chini Mwisho anamwambia Uti kuwa Meryl hasemi lolote baya kuhusu Uti,huku Uti mwenyewe akijibu kwa kusema ni kwasababu anavyowatendea wanawake.

Na anaendelea kumpasha Mwisho kuwa hadhani kama atafanya jambo baya kwao kwasababu anawaheshimu lakini Mwisho anamwambia Uti kuwa ni kwasababu wanawake anawatisha ndio maana wana muheshimu.

Katika hatu nyingine , Uti anasema Mwisho alikuwa anaongea yote hayo kwasababu alikuwa anamuhofia yeye na kuendelea kumpasha Mwisho “jitazame kwanza wewe mwenyewe halafu nitazame na mimi hutaelewa.utajikuta unanihofia ndio maana unasema mpenzi wako ananiogopa,”hayo ni maneno ya Uti.

Munya akaingilia kati na kuwaeleza kuwa Uti amewafanya watu kujihisi wanyonge na hawapi nafasi kujitutumua kwake.

Wakati hayo yakiendelea Uti akaendelea na kile alichokuwa akizungumza na Mwisho kwa kuongeza kuwa mara zote Mwisho amekuwa hana nafasi kwake ndio maana ina muuma .

Mwisho akaendelea kusisitiza kuwa washiriki wanawake wamekuwa wakimuogopa Uti kwasababu amekuwa akiwatukana na hivyo kumpa nafasi.

No comments:

Post a Comment