KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 21, 2010

KIJIJI CHA OLIMPIC NCHINI INDIA CHAWATIA MASHAKA WASHIRIKI KUSHINDWA KUKAMILIKA KWA WAKATI, UINGEREZA NA SCOTLAND WASEMA HAKINA HADHI ZA KIBINADAMU

England na Scotland watilia mashaka michuano ya madola
Uingereza pamoja Scotland wameanza kuwa katika mashaka makubwa juu ya michuano ya jumuia ya madola hususani obovu wa kijiji cha kilichoa andaliwa kwa ajili ya michuano hiyo kilichopo Delhi wakisema hakina ubora.Kwa mujibu wa taarifa zilizo ripotiwa toka kwa maafisa wa Scottland wamekaririwa wakisema makazi hayo si salama na hakufai maisha ya binadamu

Uingereza imekuwa katika kujiamini mno kuweza kufanya vizuri lakini kazi uboreshaji inapaswa kufanywa kabla ya kuanza kwa michezo hiyo October 3.
Maafisa wa Wales wako karibu na makao makuu na wanaamini kuwa waandaaji wanapaswa na wanauwezo wa kufanya hivyo.
Wawakilishi wa kwanza timu ya Ireland ya Kaskazini wanatarajiwa kuondokaa leo kuelekea India wakiwa tayari wamesha jipanga kwa ajili ya kusaka eneo mbadala endepo hali waliko pangiwa itakuwa hivyo.

Kazi ya ujenzi imekwanda tofauti na ilivyo pangwa kuelekea kwenye michuano hiyo huku ufunguzi rasmi wa kijiji hicho ukitarajiwa kufanyika alhamisi ambapo jumla ya wanamichezo 7000 na maafisa wao wakitarajiwa kufurika katika kijiji hicho.
Hali ya usalama imekuwa katika hofu kubwa hasa baada ya watu 19 kujeruhiwa baada ya daraja muhimu kuvunjika karibu na uwanja wa matukio ya kimichezo jumanne .

ARSENAL WENGER KWENDA BENCHI MCHEZO MMOJA

Chama cha kandanda nchini uingereza FA hii kimethibitsha adhabu ya bosi wa Arsenal Arsene Wenger baada ya kocha huyo kukuibaliana na maamuzi hayo ambayo kimsingi yametokana na utoaji wake wa lugha chafu na mwenendo mbaya wa kukalia benchi ambapo sasa atakuwa akitumikia adhabu ya mchezo mmoja kuwa mbali na benchi la lake.
Mfaransa huyo pamoja na adhabu hiyo atalazimika kulipa faini ya pauni elfu £8,000 ambapo atakosekana katika mchezo dhidi ya Totternham Hostspur wa League Cup hii leo.
Adhabu hiyo imetokana na mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sunderland ulipigwa katika dimba la Stadium of Light jumamosi ambapo Wenger alimkabili match officials kufuatia bao la kusawazisha la wenyeji akitoa maneno ya kupinga maamuzi ya mwamuzi.
Hata baada ya mchezo kumalizika , Wenger aliendelea kuonyesha hasira zake kwa match officials kwa kuonekana kuongeza muda wa mchezo mara baada ya zile nyingine za nyongeza za mchezo kumalizika .

BARBATOV ANASEMA ALIJIANDAA KUFANYA VIZURI TANGU SAMMER Mshambuliaji wa Manchester United Dimitar Berbatov ametanabaisha kuwa mkakati wake wa kujiweka fiki katika kipindi chote cha maandalizi ya ligi wakati wa kiangazi ndiyo siri pekee ya yeye kuwa katika kiwango ambacho anacho hivi sasa Old Trafford.
Berbatov ambaye alijiunga na United akitokea Tottenham Hotspur miaka miwili iliyopita huko nyuma alishindwa kabisa kuonyesha ubora wake kulinga na thamani yake ya ngawira za uhamisho wa pauni milioni £30.75 . alifakiwa kufunga jumla ya mabao tisa tu katika msimu wake wa uhamisho kabla ya kupachika nyavuni jumla ya mabao 12 katika msimu ulipita
Nyota huyo wa zamani wa Bulgaria hatimaye amerejesha uwezo wake katika wiki za mwanzoni mwa msimu na katika kulidhihirisha hilo katika mchezo wa jumapili dhidi ya Liverpool akafanikiwa kutingisha nyavu mara tatu yaani superb hat-trick.

Hiyo ina maana ya kwamba Berbatov mwenye umri ewa miaka 29 tayari amesha weka wavuni jumla ya mabao sita baada ya michezo mitano ya msimu huu.
Berbatov tayari ana matumaini ya kunyamazisha maneno ya ukosoaji wakati wa kuelekea katika kiangazi hususani wakati wa michuano ya kombe la dunia
Akikaririwa mwenyewe anasema
"nimefanya kazi kubwa kuwa katika kiwango sasa sina tena uzito kama ambavyo kila mtu anavyo weza kushuhudia na niweza kulifanyia kazi hilo nilikuwa nikikimbia mile sita kila siku kuelekea katika msimu mpya. Ratiba yangu ilikuwa ninashuhudia michezo ya kombe la dunia halafu naanza kukimbia halafu nakwenda kuangalia tena mchezo unaofuata kisha narejea tena kukimbia.

URENO YATHIBITISHA KUMUAJIRI PAULO BENTO KUWA KOCHA MPYA Ureno imethibitisha kumuajiri kocha wa zamani wa wa klabu ya Sporting Lisbon Paulo Bento kuwa kocha mpya wa timu ya soka ya Ureno as the new coach of the
Bento ambaye amekitumikia kikosi cha ushindi cha Ureno kama mchezaji mara 35 wakati wa enzi zake anachukua nafasi ya Carlos Queiroz, ambaye alitimuliwa kazi kutokana na matokeo mabovu na utovu wa nidhamu katika michezo ya kampeni kufuzu Euro 2012.
Baada ya Real Madrid kugomea jaribio lao la kumtaka Jose Mourinho shirikisho la kandanda la ureno FTF limemgeukia Bento kuingoza Ureno.
Bento amekuwepo katika kikosi cha Ureno miaka Euro 2000 na kombe la dunia 2002 kabla ya kuelekea kuifundisha kwa miaka minne Sporting na kufanikiwa kutwaa taji la Ureno mara mbili 2007 na 2008.
Mkataba wa Bento utamalizika 2012 huku mtihani wake wa kwanza ukiwa ni dhidi ya Denmark October 8 na atakuwa akisaidiana na Leonel Pontes na Joao Aroso kama mtaalamu wa physic na nyota wa zamani wa Sporting Ricardo Peres atakuwa kocha wa makipa.


CESC FABRIGA KUSUBIRI KWA WIKI MBILI MPAKA TATU KUFUATIA MAJEREHA Arsenal imethibitisha kuwa kiungo Cesc Fabregas atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu kufuatia mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kuwa majerahi.
Nyota huyo wa The Gunners aliumia katika kipinchi cha kwanza cha mchezo uliofanyika jumamosi dhidi ya Sunderland uliomalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 kutokana na kutokana na matatizo ya msuli.
Vipim vya scan vilivyo fanywa jana vimetanabaisha juu ya ukubwa wa tatizo lake na kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa klabu imethi bitika kuwa Cesc Fabregas atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu
Hata hivyo Fabregas hatakosekana kwa mchezo wa leo pekee dhidi ya Tottenham Hotspur lakini pia atakosekna katika mchezo ujao wa michuano ya mabingwa dhidi ya Partizan Belgrade.
Huenda pia akakosekna katika mchezo wa ligi kuu ya uingereza dhidi ya Chelsea mchezo ambao utapigwa October 3 kutegemeana kasi ya kuboreka kwa afya yake

No comments:

Post a Comment