KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 22, 2010

MWAMUZI WA MCHEZO WA KOMBE LA DUNIA ITALIA DHIDI YA KOREA KUSINI AKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

Byron Moreno ambaye alipuliza kipyenga katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2002 nchini Italia hususani mchezo kati ya Italia na Korea kusini amekamatwa kwa kuhusishwa na ubebaji wa madawa ya kulevya aina ya heroin.
Moreno raia wa Ecuador amekamatwa katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy jijini New York na maafisa wa upepelezi wanasema alikuwa na begi la madawa aina ya heroin katika nguo zake za ndani.
Afisa forodha anasema alikuwa amebeba zaidi ya zaidi ya paund kumi ya madawa hayo.
Anakumbukwa kwa kuvurunda mchezo mchezo wa kombe la dunia kati ya wenyeji wenza wa fainali za kombe la dunia Korea kusini dhidi ya Italia mchezo ambao Korea kusinia walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya italia mnamo mwaka wakorea wakipata bao la pili katika dakika za nyongeza mwaka 2002 licha ya mfungaji kuwa katika mazingira ya kuotea pamoja na kukataa penati ambayo Francesco Totti aliangushwa katika eneo la hatari na kisha kumzawadia Totti kadi nyekundu akisema alijirusha.
Mlinda mlango wa wakati huo wa Italia Gianluigi Buffon anasema
"nadhani Moreno tayari alikwisha kuwa na heroin tangu mwaka 2002,akimaanisha katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2002 lakini anasema kwa wakati ule madawa hayo yalikuwa mwilini kwake na si kwenye chupi kama ilivyo sasa yakiwa ni maneno ya dhihaka yaliyo jaa hasira.
Hata ntota wa zamani wa kikosi cha italia wakati ule Christian Panucci naye alikuwepo katika kikosi dhidi ya Korea Kusini hakuonekana kushituka baada ya kusikia taarifa hizo.
Bosi wa kikosi cha Italia cha fainali hizo za mwaka 2002 raia wa Ireland Giovanni Trapattoni anasema ashutuki na na hilo isipokuwa hiyo inathibitsha mengi ama machache yake katika katika fainali za kombe la dunia za wakati ule.


NYOTA WA SUNDERLAND TITUS BRAMBLE NA KAKA YAKE MATATANI KWA UBAKAJI


Nyota wa Sunderland Titus Bramble kizimbani kwa ubakaji .
Titus Bramble nyota wa Sunderland amelazimika kwenda kizimbani kufuatia jaribila la ubakaji ,nyota huyo amewahi kuvichezea vilabu vya Newcastle na Wigan na inaarifiwa kufanya jaribio hilo kwa mwanamke mmoja huko Newcastle .
Mlinzi huyo katika Premier League akiwa pamija na kaka yake Tesfaye Bramble walitiwa kiziwizini katika hotel ya Vermont Hotel mapema hii leo na kuhojiwa .
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 alikamatwa baada ya mwanamke huyo kuwapigia simu polisi ndani ya sekunde 20.
Sunderland Football Club haijasema lolote juu ya hilo.Bramble alijiunga na klabu hiyo akitokea Wigan katika majira ya kiangazi
Msemaji wa kituo cha polisi cha Northumbria Police amesema wanaume wawili wenye umri wa miaka 29 na 30 wamekamatwa kuhusika na ubakaji huyo.

Bramble amewahi kuichezea timu ya taifa ya uingereza chini ya umri wa miaka 21 akichezea pia vilabu vya Newcastle United na Ipswich.
Kaka yake huyo ameichezea Montserrat na Southend United pamoja na Stockport County.



CARLOS VELA NA EFRAIN JUAREZ WAKUMBANA NA ADHABU YA KIMATAIFA Mexico imewasimamisha Carlos Vela na Efrain Juarez kwa miezi sita baada ya kilo kilichoelezwa kuwa ni kuvunja sheria za uwajibikaji wao katika timu ya taifa.
Wawili hao ambao maskani yao ni nchini Uingerea pamoja na wengine kadhaa Guillermo Ochoa, Maza Rodriguez, Carlos Salcido, Andres Guardado, Gerardo Torrado, Pablo Barrera, Giovani dos Santos, Chicharito Hernandez, Rafael Marquez, Enrique Esqueda na Hector Moreno wote kwa pamoja pia wamepigwa faini ya “Pesos 50,000” ambazo ni sawa pauni elfu 2,517 ambazo pia ni sawa na dolari za kimarekani 4,000.
Adhabu hiyo inahusishwa na madai mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Colombia mchezo ambao umemalizika wakipata ushindi wa bao 1-0 mchezo ulipigwa kule Monterrey mapema mwezi huu huku Vela na Juarez ambao wanachezea katika vilabu vya Arsenal na Celtic wakivunja jumla ya sheria za kimataifa za shirikisho la kandanda nne “federation's code of conduct”.
Mkurugenzi wa timu ya taifa ya nchi yao ya Mexico Nestor de la Torre amekaririwa akisema
"Carlos Vela na Efrain Juarez watalazimika kusubiri kwa miezi sita kuanzia siku ya tukio hilo yaani September 8 kwa maana ya kutokuitwa katika national team kwa kuwa wamekuwa na makosa katika maeneo manne ."
Hata hivyo katika kipindi chote hicho inaarifiwa kuwa Mexico itakuwa na mchezo mmoja tu na mchezo wenyewe niwa kirafiki


WESLEY SNEIJDER AKAKUSHA TENA KUMFUATA JOSE MOURINHO REAL MADRID


Kiungo mchezeshaji wa Inter Milan mholanzi Wesley Sneijder amekanusha taarifa zinazo zagaa juu ya yeye kutaka kuelekea kwa kocha wake wa zamani Jose Mourinho ambaye kwasasa anakinoa kikosi cha Real Madrid ya Hispania kwa mujibu wa walaka wa kiungo huyo.
Sneijder alikuwa ndio roho ya kikosi cha Mourinho msimu wa uliopita kiasi kufanikisha mataji kadhaa ikiwemo yakiwemo ya Seria A,Copper Italia kabla ya kutwa taji kubwa la Champions League.
Baada ya kuweka kunyavu mara nane kwa kikosi katika kikosi cha Nerazzurri na kuwa ni moja ya chachu za ushindi katika kampeni za mtaji mablimbali alielekea katika michuano ya kombe la dunia akiongoza kikosi cha uholanzi ambako alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 5 na kuisaidia Oranje kufikia fainali ya konbe la dunia ambapo walipoteza mbele wa Hispania .

Mourinho ameshindwa pia kumchukua Sneijder mwenzake toka klabu hiyohiyo ya Inter Milan Maicon kuelekea Bernabeu katika usajili wa kingazi lakini wakala wa mduchi huyo Soren Lerby ametanabaisha kuwa 'Special One' pia anafikiria kumrejesha wakala wake katika klabu hiyo ambayo haiikuuza wachezaji msimu wa usajili uliopita.
Na wakati mazungumzo ya mkataba kuelekea kukamilika Lerby anasema wakati Sneijder akifurahia maisha ndani ya San Siro uwezekano wa Mourinho ambaye yuko Real Madrid kurejea limekuwa ni swali


NEYMAR AMFUKUZISHA KAZI KOCHA WAKE WA SANTOS KISA PENATI Timu ya Santos ya nchini Brazil imemfukuza kocha wake mkuu Dorival Junior baada ya kuzozana na nyota wa kikosi Neymar.
Santos imefikia maamuzi hayo ya kumswaga kocha huyo Dorival Junior na kuthibitshwa na klabu yenyewe kupitia mtandao maalum wa klabu .
Kocha huyo amekuwa katika mzozo na nyota huyo tangu juma lililopita kufuatia Neymar kutaka kupiga penati lakini Dorival Junior akamueleza mshambuliaji huyo kuwa penati hiyo itapigwa na Marcel.
Baadaye Neymar aliondoka na kisha kwa hasira baadaye alimvaa kocha wake Dorival katika benchi la Santos na kiasi kupelekea mwamuzi wa pembeni kumtuliza baada kocha wake kumdharau.
Baadaye Neymar aliomba radhi wa ufedhuli wake lakini Dorival Junior lakini alionekana kutokubaliana naye na kulazimika kumuadhibu kwa kumtoa katika kikosi kuelekea katika mchezo wa leo dhidi ya Corinthians katika dimba la Sao Paulo clasico Wednesday.

Bodi ya wakurugenzi ya Santos wameonekana kutokufurahishwa na maamuzi ya Dorival na kulazimika kumuondosha kocha huyo wa kiwango cha juu nchini humo.
Taarifa ya mtandao wa klabu inasomeka Marcelo Martelote ameteuliwa kuchukua nafasi mpaka pale atakapo patikana mbadala wake wa kudumu.

No comments:

Post a Comment