KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 23, 2010

UINGEREZA BADO KIGUGUMIZI KUELEKEA NEW DELHI KWA AJILI YA MICHUANO YA MADOLA WAKITAKA UHAKIKA WA USALAMA NA MAKAZI BAADA YA MAANDALIZI KUELEKEA KWENYE MICHUANO HIYO KUTOKAMALIKA KWA WAKATI HUKU DARAJA KARIBU NA UWANJA MKUBWA WA MICHUANO KUJERUHI WATU 23.Chini katika picha ni daraja lililovunjika

England bado kuamua kutuma kikosi chake cha kwanza katika michuano ya jumuia ya madola alhamisi hii licha ya hali ya wasiwasi juu ya kukamilika kwa maandalizi ya michezo hiyo.
Mwenyekiti wa England Sir Andrew Foster amekaririwa akisema bado wanahitaji uhakiki wa kiusalama kwa wanamichezo wao hususani juu ya makazi na mazingira kamili ya maeneo ya kuchezea michezo yenyewe.
Akiongeza Foster anasema timu yao bado ina dhamira yakuelekea Delhi na kusema hawajabadili msimamo wa kuelekea huko.
"timu yetu inaendelea kujiandaa kwa kikosi cha kwanza kuelekea Delhi kwa kikosi cha kwanza kufanya safari kikiwa na wanamichezo ambao wanaondoka alhamisi."
"bado tunaamini kuwa hali ya maandalizi si safi na tunafuatilia na viongozi wetu wa huko kabla ya kuondoka.

Takrinani wa 23 people wamejeruhiwa katika daraja kubwa linalotumiwa zaidi na watembea kwa miguu katikati ya mji wa Delhi karibu na uwanja mkubwa utakao tumika kwa ajili ya michezo ya olimpic ajali hiyo imetokea hapo jana.
Scotland, Wales na Uingereza tayari wameonyesha wasiwasi wao juu ya ushiriki katika michuano hiyo mwezi ujao kwa kuhofia juu ya vifaa na hali ya usalama ndani ya mji huo wa Delhi.
Timu za Scotland na Jersey zinachelewa kuelekea India kwa hofu ya kijiji cha wanamichezo kuwa na matatizo.
Wales kwa upande wake imetoa muda kwa waandaaji kuwa mpaka kufikia jumatano usiku wa leo kuthibtisha kuwa viwanja vyote viko tayari ilhali waingereza wakisema hali ya ipo katika hali ya kama ncha ya kisu.

Michuano ya madola inatarajia kuanza Octoba 3 mpaka octoba 14 na wanamichezo wakianza kuwasili India juma hili .
Mataifa mbalimbali yamelalamikia juu ya makazi yao watakapo kuwa huko wakisema ni "unfit for human habitation" ilhali wasiwasi wa kiusalama umeendelea kuwatisha kwa kuwa ndani ya majengo dari za majengo ama lugha nyepesi “ceiling body” hazina ubora na mfano mkubwa ni kudondoka kwa sehemu ya ceiling bodi ya uwanja wa mashindano hii leo.
Hakuna majeruhi aliyeripotiwa kufuatia tukio hilo maafisa wa India wamethibtisha hilo na wakisema hilo sia jambo la kuwatisha washiriki.
Scotland kama sehemu ya washiriki wa kwanza kuelekea huko wakiwa na jumla ya wanamichezo 41 kwa michezo ya boxing, rugby na wrestling wanatarajia kuelekea huko kesho lakini wasiwasi wa hali ya mambo umekuwa kikwazo kutoa taarifa ni lini hasa watakwea pipa kuelekea huko.

ARSENE WENGER KUENDELEA KUFUNDISHA KWA MUDA MREFU Arsene Wenger amesisitiza kuwa atasalia katika kazi ya ukocha kwa muda muda mrefu lakini anafikiria kurejea nyumbani kwao nchini Ufaransa baada ya maktaba wake na Arsenal utakapo malizika mwaka 2014.
Kwasasa Wenger ana umri wa miaka 61 akiwa tayari ameshaongeza mkataba wake na klabu yake ya Arsenal kwa muda wa miaka mitatu na huku akisema anafarijika sana kufanya kazi ndani ya viunga vua uwanja wa Emirates Stadium.
Kuna uwezekano wa Wenger kurejea nyumbani kwa alikozaliwa na inafikiriwa kuelekea huko Strasbourg sehemu ambako aliwahi kucheza soka.

No comments:

Post a Comment