KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 30, 2011

Ajax yathibitisha kimsingi kukubaliana na Roma kwa ajili ya Maarten Stekelenburg Klabu ya AS Roma hatimaye imekubaliana na Ajax kwa ajili ya mlinda mlango wake Maarten Stekelenburg kuhamia katika klabu hiyo ya Uholanzi.
Taarifa iliyotolewa na kupitia katika mtandao wa Ajax imesomeka kuwa makubaliano kati ya vilabu hivyo viwili ni katika kukamilisha baadhi ya masharti bila ya kutaja masharti hayo.
Wakati huo huo kulingana na taarifa kupitia gazeti la Corriere dello Sport ni kwamba Stekelenburg tayari ameshawasili katika jiji la Rome na pinde tu atafanyiwa vipimo vya afya yake kabla ya majadiliano juu ya haki zake binafsi ndani ya klabu yake hiyo mpya.
Taarifa ndani ya Italy na nyingine toka Uholanzi zinasema Roma italazimika kutoa euro milioni €6 kumalizia huduma nyingine mbalimbali za mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28.
Stekelenburg ameichezea uholanzi jumla ya michezo 40 ya kimataifa na ameichezea Ajax jumla ya michezo 282.

No comments:

Post a Comment