KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 15, 2012

Bonface mkwasa:mwanahamisi anastahili tuzo.

kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars ) Charles Bonface Mkwasa amepongeza tuzo ya mchezaji bora wa soka la wanawake mwaka 2011 iliyochukuliwa na Mwanahamisi Omari maarufu kama "Gaucho" tuzo ambazo zimeandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini (TASWA)
Bonface amesema mwanahamisi alikuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo na amefunga magoli mengi ambayo yameisaidia timu katika mashindano mbalimbali.

Bonface amsema tuzo hiyo itaamsha hari kwa wachezaji wengine katika timu ya taifa na vilabu mbalimbali na kuusukuma mbele mpira wa wanawake nchini Tanzania.

Mwanahamisi amewashinda wenzake akina Asha Rashid maarufu kama Asha mwalala, Fatuma Mustafa na Etoo Mlezi.
Bonface mkwasa ambaye anakifundisha kikosi cha timu ya Twiga amesema tuzo hiyo ya Mwanahamisi ichukuliwe kama changamoto kwa wadau kulisaidia soka la wanawake nchini kwani kwa kufanya hivyo kutaibua hamasa kubwa kwa vijana zaidi wa kike kuupenda mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Kwa upande wake Mwanahamisi "Gaucho" akizungumza na Rockersports amesema anamshukuru mungu kwa kupata tuzo hiyo kwa kuwa maisha yake ya soka yalianza katika mazingira ya utata mkubwa kiasi mpaka kufukuzwa na wazazi nyumbani kwa kukataa shule na na kujiunga na soka wakati huo akijunga na timu ya soka ya wanawake ya Mburahati Queens ya Mburahati.

 Mwanahamisi amesema ilikuwa kazi kwa wazazi wake kukubali kile alichokuwa anakitaka na alilazimika kuishi maisha ya Geto na wachezaji wenzake wa timu ya Mburahati Queens mwaka wa 2006 kabla ya mwaka mmoja baadaye yaani 2007 kupata bahati ya kujiunga na timu ya Taifa ya Twiga Stars ambayo mpaka sasa imebadili maisha yake.

Mwanahamisi anasema ataitumia tuzo hiyo kama changamoto kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo wake wa soka ambao amesema anaupenda sana ili kuweza kufikia malengo yake ya kucheza soka la kulipa zaidi.
Aidha amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumpa ushirikiano mkubwa huku akimpongeza kocha wa Twiga stars Charles Bonface Mkwasa kwa mchango mkubwa wa kimafunzo anaoupata toka kwake na uvumilivu wake katika kundisha timu hiyo ya taifa ya wanawake ya Twiga.

No comments:

Post a Comment