KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 15, 2012

Timu ya taifa ya Rwanda Amavumbi imeondoka leo kuelekea Nigeria bila ya Uzamukunda


Kocha wa Timu ya taifa Rwanda (Amavumbi) Milutin Sredojovic ameendelea kulinda kikosi chake kile kile kwa ajili ya mchezo wao wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Nigeria
Hata hivyo kikosi hicho kitamkosa mshambuliaji wa AS Cannes Elias Uzamukunda ambaye ameachwa hapo jana katika kikosi cha timu hiyo kilichoelekea Calabar katika mji wa Canaan.

 Uzamukunda ambaye aliponya majeraha yake ya mguu wiki iliyopita wakati timu ya Rwanda ilipokwenda sare ya bao 1-1dhidi ya Benin kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia katika uwanja wa Amahoro nchini Rwanda, ameshindwa kumuhakikishia daktari wa timu hiyo uhakika wa kupona kabisa.

Mbali ya Uzamukunda, mchezaji wa APR Ismail Nshutiyamagara ,kiungo wa SC Kiyovu Hussein Sibomana na mlinda mlango wa Isonga Olivier Kwizera kocha wa kikosi hicho ameendelea kulinda kikoso chake kile kile kwa ajili ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Super Eagles ambao walikwenda nao sare ya bila kufungana katika mchezo wao wa kwanza mwezi February mjini Kigali mwezi February.
 Rwanda squad-: Fabrice Twagizimana, Jean Claude Ndoli, Meddie Kagere, Salomon Nirisarike, Haruna Niyonzima, Tumaine Ntamuhanga, Eric Gasana, Jean Baptista Mugiraneza, Olivier Karekezi, Bokota Labama, , Imran Nshimiyimana.
 Jean Claude Iranzi, Steven Godfroid, Dady Birori, Emery Bayisenge, Evaritse Mutuyimana, Ndaka Frederique na Jonas Nahimana

No comments:

Post a Comment