Baada ya
kutangazwa kuwa mrithi wa Guardiola mwezi April, kocha msaidizi wa zamani wa Barcelona
rasmi ametiliana saini na klabu hiyo kuwa kocha wa kudumu lakini hata hivyo
amekataa kufananishwa na mtangulizi wake.
Meneja mpya
wa Barcelona Tito Vilanova hii amesaini mkataba wa miaka miwili na kigogo hicho
cha nchini Hispania kuchukua nafasi ya Pep Guardiola.
Ilitaangazwa
mwezi April wakati Guardiola aliyeicha timu hiyo akishinda mataji 14 kuwa
atarithiwa na msaidizi wake Vilanova.
Baada ya
mkutano na wanahabari kutangaza juu ya kutia saini hii leo Vilanova amemshukuru
mtangulizi wake ambaye alimfahamisha kuwa yuko katika mstari wa kuelekea kuwa
kocha mkuu baada ya kichapo cha ligi ya mabingwa toka kwa Chelsea.
Akizungumza
na FCB Live, Vilanova amesema
"namshukuru Guardiola, rafiki yangu
alikuwa kama kaka yangu. Imekuwa ni faraja kuwa pembeni yake kwa kipindi cha takribani
miaka mitano.
"baada
ya mchezo dhidi ya Chelsea Guardiola alinieleza kuwa anataka kupumzika na kuna
uwezekano wa klabu kunipa offer ya kazi.
"kwanza
nilishangaa sikuwahi kusikia chochote kuhusu hilo huko nyuma na klabu
iliponithibitisha ilichukua siku kadhaa kufikiria juu ya hilo."
Akiwa hajawahi
kuingoza timu yoyote huko nyuma , Vilanova anadhani huenda akaendelea kusalia
upande wa Guardiola.
Ameonekana kuchukuzwa
na kulinganishwa na mtu ambaye Vilanova ametengeneza jina kwake kama msaidizi
na ametaka asifananishwe na Guardiola.
No comments:
Post a Comment