Bin Hammam |
Nchi ya Qatari
imepata ahueni ya kuendelea na kifungo cha maisha katika kujishughulisha na
mambo ya mpira wa miguu kufuatia kushinda rufaa yake ya kupinga kufungiwa
maisha kujishulisha na mchezo huo adhabu ambayo ilitolewaFIFA mwaka uliopita.
Mohamed Bin
Hammam ambaye ni mwenyekiti wa soka nchini Qatar na aliyekuwa mjumbe wa kamati
ya utendaji ya fifa alipata adhabu ya kutojihusisha na soka maisha lakini alikata
rufaa katika mahakama ya usuluhishi ya michezo duniani (CAS) kupinga adhabu
hiyo.
Qatari ilionekana
kuwa na kosa kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa maafisa wa soka wa Caribbean kwa
lengo la kupambana na Sepp Blatter kuwania nafasi ya Rais wa FIFA na Bin Hammam
akiwa ndiye mpinzani wake mkubwa.
Bin Hammam mara
zote alikuwa akikanusha tuhuma hizo na sasa imethibitishwa na CAS, ambayo
imesema wameshindwa kupata ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma hizo dhidi yake.
No comments:
Post a Comment