KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 19, 2012

'KING KIBADENI MPUTA' NA SALUM KANONI KUIPIGA TAFU KAGERA SUGAR MSIMU UJAO.

Abdalah Kibadeni(King Kibadeni Mputa)
 Timu ya kagera sugar inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara katika kuhakikisha inaboresha benchi lake la ufundi imeamua kuongeza nguvu kwa kumchukua aliyekuwa kocha wa vijana wa Simba Abdalah Kibadeni(King Kibadeni Mputa) 

Akiongea na Rockersports kocha msaidizi  wa timu hiyo Mlage Kabange amesema timu yake inatarajia kuingia kambini tarehe 20/07/2012 tayari kwa kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kwamba Kibadeni atakuwa anachukua mikoba ya kocha wa zamani mganda Jackson Mayanja.
Kabange amesema katika kuboresha kikosi chao msimu ujao Kagera Sugar pamoja na kumchukua Kibadeni lakini pia imemsajili mlinzi wa kulia wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba Salum Kanoni.
Kagera sugar  pia imewasajili wachezaji wawili wa kigeni toka nchini Nigeria, Benjamin Efee na Willfred Emee na kumchukua mshambuliaji Daringtomi Enina toka Toto Afrika ya Mwanza.
Mlinzi wa zamani wa Simba Salum Kanoni
 

No comments:

Post a Comment